Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Waziri Ummy: Serikali isiwe kikwazo

TAASISI za serikali zinazohusika na masuala ya ukaguzi na udhibiti wa bidhaa, zimetakiwa kutokuwa kikwazo kwa maendeleo ya wajasiriamali na ujenzi wa viwanda hapa nchini. Anaripoti Regina Kelvin…(endelea).

Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akihutubia kwenye mkutano wa wadau wa kujadili mchango wa taasisi za serikali katika kuanzisha na kuboresha viwanda vya chakula nchini.

Waziri Ummy amesema Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kusikilizana katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuondoa vikwazo kwa wajasiriamali na ujenzi wa viwanda.

“TBS, TFDA na mamlaka nyingine inabidi msikilizane ili kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara na wawekezaji,” amesema.

Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema serikali itanedelea kuondoa changamoto za wajasiriamali na wawekezaji wa viwanda, lakini amewataka wajasiriamali hao kutobweteka katika uzalishajiwa bidhaa zenye ubora.

“Tunajenga vianda kwa ajili ya kutoa ajira, kuanzisha bishaa zenye ubora na viwango vya kukidhi matakwa ya watanzania na soko la nje ya nchi. Tunachopaswa kufanya tutengeneze viwango vya kiuhalisia. Tunawasaidia lakini Msibweteke,” amesema.

TAASISI za serikali zinazohusika na masuala ya ukaguzi na udhibiti wa bidhaa, zimetakiwa kutokuwa kikwazo kwa maendeleo ya wajasiriamali na ujenzi wa viwanda hapa nchini. Anaripoti Regina Kelvin…(endelea). Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akihutubia kwenye mkutano wa wadau wa kujadili mchango wa taasisi za serikali katika kuanzisha na kuboresha viwanda vya chakula nchini. Waziri Ummy amesema Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kusikilizana katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuondoa vikwazo kwa wajasiriamali na…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube