Cecilia Augustino Mwanga wa Demokrasia Makini

Wagombea 10 waliochukua fomu urais Tanzania 

Spread the love

WAGOMBEA kumi wa urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 wamechukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Fomu hizo zimeanza kutolewa tarehe 5 Agosti, 2020  Ofisi za NEC zilizopo nje kidogo ya Jiji la Dodoma eneo la Njedengwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage.

Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo, utahitimishwa tarehe 25 Agosti 2020, siku ambayo NEC itawateua waliokidhi vigezo vya kuteuliwa.

Hadi kufikia leo Jumamosi tarehe 8 Agosti, 2020, wagombea kumi wamekwisha kuchukua fomu hizo kati yao wanawake ni wawili.

Vyama vilivyochukua fomu hizo ni;  Seif Maalim Seif (AAFP) na mgombea mwenza, Rashid Ligania Rai, Leopard Mahona wa NRA, Philip John Fumbo wa DP,  Rais John Pombe Magufuli wa CCM na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan na Tundu Lissu wa Chadema na mgombea mwenza, Salum Mwalimu

Wengine ni; Mutamwega Bati Mgaiwa wa SAU,  Qeen Cuthbert Sendiga wa ADC, Twalib Ibrahim Kadege kupitia UPDP, Cecilia Augustino Mwanga wa Demokrasia Makini, Bernard Membe wa ACT- Wazalendo  na mgombea mwenza wake, Profesa Omar Fakih Hamad.

Qeen Cuthbert Sendiga-ADC

Tundu Lissu-Chadema

Bernard Membe-ACT-Wazalendo

Dk. John Magufuli-CCM

Leopard Mahona-NRA

Seif Maalim Seif (AAFP)

Philip John Fumbo-DP

Mutamwega Bati Mgaiwa wa SAU

Twalib Ibrahim Kadege (kulia)-UPDP

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

WAGOMBEA kumi wa urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 wamechukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Fomu hizo zimeanza kutolewa tarehe 5 Agosti, 2020  Ofisi za NEC zilizopo nje kidogo ya Jiji la Dodoma eneo la Njedengwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage. Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo, utahitimishwa tarehe 25 Agosti 2020, siku ambayo NEC itawateua waliokidhi vigezo vya kuteuliwa. Hadi kufikia leo Jumamosi tarehe 8 Agosti, 2020, wagombea kumi wamekwisha kuchukua fomu hizo kati yao wanawake ni…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!