JESHI la Polisi mkoani Tanga, linawashikilia wafanyabaishara 12 wanaodaiwa kufanya biashara ya ubadilishaji fedha za kigeni bila leseni ya biashara hiyo kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Wafanyabaishara hao walikamatwa katika msako mkali uliofanywa na vyombo vya dola katika maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, na maeneo mbalimbali mkoani humo.
Leons Rwegarisa, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tanga akizungumza na wanahabari tarehe 7 Agosti 2019, amesema jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa hao wakiwa na fedha kiasi cha Sh. 63.3 Milioni na Dola za Marekani 65,961.
Kamanda huyo ameeleza, wafanyabiahsra hao wanahojiwa na kwamba uchunguzi wa tuhuma zao ukimalika, watachukuliwa hatua za kisheria.
Wakati huo huo, Kamanda Rwegasira amesema, kwenye operasheni hiyo, jeshi hilo limekamata Paundi ya Uingereza 400, Randi ya Afrika Kusini 1,2020, Euro 270, Shilingi ya Uganda 2,000 na ya Kenya 236,549.
Leave a comment