Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyabaishara 12 wakamatwa wakiwa na mamilioni ya fedha
Habari Mchanganyiko

Wafanyabaishara 12 wakamatwa wakiwa na mamilioni ya fedha

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Tanga, linawashikilia wafanyabaishara 12 wanaodaiwa kufanya biashara ya ubadilishaji fedha za kigeni bila leseni ya biashara hiyo kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wafanyabaishara hao walikamatwa katika msako mkali uliofanywa na vyombo vya dola katika maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, na maeneo mbalimbali mkoani humo.

Leons Rwegarisa, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tanga akizungumza na wanahabari tarehe 7 Agosti 2019, amesema jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa hao wakiwa na fedha kiasi cha Sh. 63.3 Milioni na Dola za Marekani 65,961.

Kamanda huyo ameeleza, wafanyabiahsra hao wanahojiwa na kwamba uchunguzi wa tuhuma zao ukimalika, watachukuliwa hatua za kisheria.

Wakati huo huo, Kamanda Rwegasira amesema, kwenye operasheni hiyo, jeshi hilo limekamata Paundi ya Uingereza 400, Randi ya Afrika Kusini 1,2020, Euro 270, Shilingi ya Uganda 2,000 na ya Kenya 236,549.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!