April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali, Green Miles wavutana

Lake Natron (East)

Spread the love

WAKATI serikali ikieleza kufuta umiliki wa kitalu cha uwindaji wa kitalii cha Lake Natron (East), kilichokuwa kinamilikiwa na Kampuni ya Uwindaji wa Kampuni ya Green Miles, kampuni hiyo imeeleza kuendelea kufanya shughuli zake. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Serikali kupitia Dk Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii ndiye aliyefuta umiliki wa kitalu hiyo kutokana na kile kilichoelezwa ‘kwa maslahi ya taifa’.

Tarehe 7 Agosti 2019 Dk. Kigwangalla alitoa taarifa ya kufuta umiliki wa kitalu hicho, akisema kwamba hatua hiyo imechukuliwa ili kulinda maslahi mapana ya taifa, baada ya uchunguzi wa kina kufanyika sambamba na kupatikana kwa taarifa za kiintelijensia.

Hata hivyo, taarifa ya Dk. Kigwangalla haikuweka wazi sababu za kufuta usajili wa kitalu hicho, bali ameeleza kwamba alifanya uamuzi huo baada ya kupokea ushauri wa watalaamu.

 “Baada ya uchunguzi wa kina na ufuatiliaji, na pia kupokea taarifa za kiintelijensia na kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa na ya wana-Longido, nimetafakari kwa kina na kupokea ushauri wa wataalamu, hatimaye kufikia uamuzi wa kufuta umiliki wa kitalu hiki. #MzeeWaField #HK,” ameandika Dk. Kigwangalla katika ukurasa wake wa Twitter.

Kufuatia sakata hilo, Kampuni ya Green Miles imetoa taarifa kwa umma, ikidai uamuzi huo wa Dk. Kigwangalla ni muendelezo wa mkakati wa kuichafua kampuni hiyo na kuiharibia biashara yake.

Kampuni hiyo imeeleza, itaendeleza shughuli zake za uwindaji wa kitalii kama kawaida kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi, kwani haijapokea taarifa yoyote kuhusu kufutiwa usajili kutoka serikalini.

“Kampuni yetu inapenda kuufahamisha umma wa Tanzania, watalii wetu na mawakala wao walio ndani na nje nchi,  kuwa taarifa hizo sio za kweli. Kwa taarifa hii tunawajulisha wote walioguswa na kadhia hii kuwa shughuli za uwindaji wa kitalii za kampuni yetu zitaendelea kama kawaida.

 Kwenye ukurasa wake wa twitter leo tarehe 8 Agosti 2019, Dk. Kigwangalla ameandika: “Mtu anakanusha utafikiri anajipa yeye hicho kitalu. Waziri mwenye mamlaka ya kugawa vitalu amefuta umiliki wake, anabisha vipi sasa. Mwenye kitalu kachukua, wewe unakataa!

https://twitter.com/HKigwangalla/status/1159397685130137600

error: Content is protected !!