Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Wabunge kuminyana uchaguzi Simba
Michezo

Wabunge kuminyana uchaguzi Simba

Juma Nkamia
Spread the love

KAMATI ya uchaguzi ya klabu ya Simba imewapitisha Juma Nkamia na Murtaza Mangungu kuwania nafasi ya Mwenyekiti katika uchaguzi mdogo wa klabu hiyo mara baada ya kupita katika michakato yote. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Uchaguzi huo ambao utafanyika tarehe 7 Februari, 2021 ambao utakuwa wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Swedi Nkwabi ambaye alijiuzuru katika nafasi hiyo 14 septemba 2019.

Wagombea hao ambao walikuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania katika muhura uliopita ambao Juma Nkamia akiwakilisha jimbo la Chemba (CCM) lililopo Dodoma, huku Murtaza Mangungu akiwakilisha jimbo la Kilwa Kaskazini.

Akitangaza majina hayo mbele ya waandishi wa habari leo tarehe 16 Januari, 2021 kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Boniface Lihamwike alisema kuwa wawili hao wamepitishwa kutokana na wagombea wawili kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na sababu zao binafsi mara baada ya kupitia kwenye hatua ya pingamizi.

“Wakati tukiwa na wagombea hawa wanne kamati yangu ilipokea barua kutoka kwa wagombea wawili ambao ni Rashidi Shangazi pamoja na Hamisi Omari wakiomba kujiengua kwenye mchakato huu kwa kuwa sehemu ya wagombea,” alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha Lihamwike aliendelea kwa kusema kuwa mara baada ya kuleta maombi hayo ya kutaka kujiengua kwenye uchaguzi huo kamati ilikaa na kuwapa majibu ya kukubali maombi yao kwa kuwa ni jambo lililopo kwenye kanuni.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo aliwataka wanachama wa klabu ya Simba kuwapa ushirikiano wagombea hao na kuwataka kufanya kampeni za kistaarabu huku wakizingatia kanuni za uchaguzi na sheria za nchi na kama kuna mgombea akikiuka kanuni hizo atachukuliwa hatua stahiki.

Murtaza Mangungu

“Nawahasa wagombea hawa ambao wamepita, kufanya kampeni kistaarabu kwa kuzingatia sheria za nchi na kanuni za uchaguzi na kamati yangu haitasita kumchukulia mgombea hatua kama atakwenda tofauti na taratibu,”  aliongezea Mwenyekiti huyo.

Toka kuanza kwa mchakato huo wa uchaguzi ndani ya Simba toka tarehe 13 Desemba, 2020 wanachama waliojitokeza kuchukua fomu walikuwa 11 na fomu zilizorejeshwa zilikuwa saba, na mara baada ya kamati hiyo kufanya upembuzi walifanikiwa kupitisha majina matono.

Kampeni za uchaguzi huo zitadumu kwa siku 21, ambazo zinaanza kuanzia siku ya kesho tarehe 17 Januari, 2021 mpaka tarehe 6 Februari, 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!