May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbatia: Katiba mpya ni lazima, hatutapiga magoti

James Mbatia

Spread the love

CHAMA cha siasa cha upinzani nchini Tanzania, NCCR-Mageuzi “Katiba Mpya ni takwa la lazima kwa Watanzania, penda usipende.” Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo, imetolewa leo Jumamosi tarehe 16 Januari 2021 na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

Madai hayo ya NCCR-Mageuzi, ni sawa na yanayotolewa na wadau wengine wa demokrasia ya kutaka Katiba Mpya kwa kufufua mchakato uliokwama mwaka 2015.

Mchakato wa Katiba Mpya uliishia kura ya maoni iliyokuwa ifanyike Aprili 2015, iliahirishwa kwa kigezo kwamba, uboreshaji wa daftari la kudumu uliokuwa ukifanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutokamilika.

Hata hivyo, mpaka sasa, kuna Katiba Inayopendekezwa ambayo wadau wamekuwa wakiipinga na kutaka mchakato ufufuliwe kwa kuanzia Rasmi ya Pili ya Katiba Mpya iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) amesema, “Katiba mpya ni lazima kwa Watanzania, penda usipende. Ili Watanzania tuwe na amani, furaha lazima iwe kwenye mwanga na si giza na hii ni Katiba mpya ambayo haiepukiki.”

“Katiba mpya ni lazima, pende tusipende, hatuombi Bunge, Mahakama au Serikali, ni haki ya Watanzania. Hatuhitaji kupiga magoti kuomba Katiba Mpya. Tutashirikiana na kila mmoja bila kuangalia itikadi za vyama na kila mtu ili tupate Katiba mpya,” amesema Mbatia

Katika hotuba yake, Mbatia amekumbushia machungu ya uchaguzi mkuu uliopita wa tarehe 28 Oktoba 2020 akisema, ni vigumu kuelezea kuwa ulikuwa wa haki na usawa wakati kuna vitendo vilivyofanyika ambavyo si vya kuvumilika.

Mbatia amesema, waandishi wa habari walitumika kufikisha taarifa mbalimbali, lakini ulipowadia wakati wa uchaguzi wenyewe, wakakutana na vikwazo kadhaa ikiwemo kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.

“Unatumia waandishi wa habari vizuri kupeleka taarifa zako, lakini wakati wa uchaguzi mkuu unazima mitandao ya kijamii, sasa kwa nini kampeni zinakuwa kwenye mwanga ila siku ya uchaguzi unakuwa gizani, mtindo huo unasemaje kuna uwazi,” amehoji Mbatia aliyeshindwa kutetea ubunge wa Vunjo

error: Content is protected !!