Usajiri wamrudisha Van Der Sar Manchester

EDWIN Van Der Sar, mlinda mlango wa zamani wa Manchester United ni moja kati ya majina matatu yaliotajwa kuja kukalia kiti cha Mkurugenzi wa Michezo ndani ya klabu hiyo kufuatia kushindwa kufanya vizuri katika dirisha kubwa la usajiri, majira ya joto. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Majina mengine yaliotajwa katika kinyang’anyiro hicho ni Ramon Rodriguez Verdejo ambaye ni mkurugenzi wa sasa wa michezo wa klabu ya As Roma inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia ‘Seria A’ pamoja na Fabio Paratic.

Manchester United mpaka dirisha la usajiri linafungwa walifanikiwa kunasa saini za wachezaji wawili tu, kiungo kutoka Brazir Frederico Rodrigues na Diogo Dalot ambaye ametoka klabu ya FC Porto ya Ureno huku timu hiyo ikionekana kuwa na mapungufu makubwa hasa katika eneo la ulinzi na kupelekea watu wengi kutoipa nasafi ya kufanya vizuri katika msimu huu.

Kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho pamoja na naibu mwenyekiti Ed Woodward watashirikiana kuhakikisha wanapata mtu sahihi kwenye nafasi hiyo ili waweze kufanya vizuri katika dirisha dogo la usajiri mwezi januari.

EDWIN Van Der Sar, mlinda mlango wa zamani wa Manchester United ni moja kati ya majina matatu yaliotajwa kuja kukalia kiti cha Mkurugenzi wa Michezo ndani ya klabu hiyo kufuatia kushindwa kufanya vizuri katika dirisha kubwa la usajiri, majira ya joto. Anaripoti Kelvin Mwaipungu ... (endelea). Majina mengine yaliotajwa katika kinyang’anyiro hicho ni Ramon Rodriguez Verdejo ambaye ni mkurugenzi wa sasa wa michezo wa klabu ya As Roma inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia ‘Seria A’ pamoja na Fabio Paratic. Manchester United mpaka dirisha la usajiri linafungwa walifanikiwa kunasa saini za wachezaji wawili tu, kiungo kutoka Brazir Frederico Rodrigues na Diogo Dalot…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Masalu Erasto

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram