Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TLS ya Lissu yahaha kujiokoa na kitanzi
Habari Mchanganyiko

TLS ya Lissu yahaha kujiokoa na kitanzi

Tundu Lissu, Rais wa TLS
Spread the love

CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimeitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama, ikiwa ni jitihada za kutaka kujiokoa na ‘rungu’ la serikali, anaandika Shafiyu Kyagulani.

Katika ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam, mawakili wa Tanganyika wanakutana chini ya mwenyekiti wao Tundu Lissu, ili kuijadili hatma ya chama hicho hususan baada ya kusudio la serikali kukifuata kupitia mapendekezo wa marekebisho ya sheria uliowasilishwa hivi karibuni.

Mbali na kuwa Rais wa TLS, Lissu pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

“Tunakutana kwa sababu kwa miaka 63 tangu kuanzishwa kwa TLS, kwa wakati huu ndiyo tupo kwenye hatari zaidi ya kufutiwa usajili wetu wa kisheria na kupokwa ukuru wetu wa kufanya kazi.

“Tumekuwa tukifanya kazi kwa uhuru na kwa kizingatia weledi wa kitaaluma kwa muda mrefu lakini kupitia mapendekezo ya marekebisho ya kisheria yanayotarajia kuwasilishwa na serikali, tutakuwa chini ya udhibiti mkali wa dola kuliko wakati mwingine wowote,” amesema Lissu katika taarifa yake kwa mawakili.

Serikali inapendekeza kuanzishwa kwa Bodi ya Usajili wa Mawakili nchini ambayo ndiyo itakuwa na mamlaka ya kuandikisha mawakili na hata kuwafutia usajili, jambo ambalo linaelezwa kuwa ni tishio jipya la uhuru wa mawakili na hata uhuru wa mahakama.

Mpango wa Serikali kukifuata Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) ulitangazwa mapema mwaka huu na Dk. Harrison Mwakyembe aliyekuwa waziri wa Sheria na Katiba, ambapo pamoja na mambo mengine alikishutumu chama hicho kwa kutaka kujigeuza chama cha siasa.

“Sitasita kupeleka muswada Bungeni ili kuifutia usajili TLS na kuiombea usajili kwa Msajili wa Vyama vya Siasa,” alionja Dk. Mwakyembe katika mkutano wake na viongozi wa juu wa TLS wa wakati huo akiwemo John Seka, Rais wa TLS kabla ya Lissu.

Dk. Mwakyembe alitoa kauli hiyo katika kipindi cha mchakato wa uchaguzi wa TLS ambapo wagombea wengi walijitokeza akiwemo Lawrance Masha, Victoria Mandari, Francis Stolla na Tundu Lissu.

Lissu aliibuka na ushindi wa zaidi ya asilimia 80 katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC Mjini Arusha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!