Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge wa Chadema azua jambo
Habari za Siasa

Mbunge wa Chadema azua jambo

Gari ya Zimamoto
Spread the love

FRANK Mwakajoka, Mbunge wa Jimbo la Tunduma mkoani Songwe, amesababisha vicheko na miguno ndani ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma, baada ya kuisifia serikali ya Zambia kwa msaada mkubwa inaotoa jimboni kwake ilihali serikali ya Tanzania ikijikita katika kukusanya kodi tu, anaandika Dany Tibason.

Katika kipindi cha maswali na majibu kwa wizara mbalimbali Mwakajoka amesema serikali ya Zambia imekuwa ikitoa gari la zimamoto kwa ajili ya wananchi wa Tunduma, ilihali wananchi hao wamekuwa wakilipa ada ya zimamoto kwa serikali ya Tanzania bila kupata huduma hiyo.

“Kila yanapotokea majanga ya moto katika mji wa Tunduma nchi ya Zambia imekuwa ikitoa gari ya zimamoto, naomba kutoa shukrani zangu kwa serikali ya Zambia kwa kuona umuhimu wa kutuazima gari la zimamoto pale linapohitajika.

“Je, kwa kuwatoza ada ya zimamoto wananchi wa mji wa Tunduma wakati hakuna huduma hiyo na badala yake wanaipata kwa msaada wa serikali ya Zambia, je hiyo si dhuluma inayofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi?” amehoji Mwakajoka.

Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akijibu swali hilo amesema ni kweli katika halmashauri ya mji wa Tunduma hakuna gari la zimamoto huku akieleza kuwa;

Ada zinazotozwa na jeshi la zimamoto na uokoaji ni kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Zimamoto Na. 14 ya mwaka 2007 na kanuni za ukaguzi za mwaka 2008 na marekebisho yake ya mwaka 2012/14.

“Hata hivyo, katika Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Halmashauri ya Tunduma ina kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambacho kipo katika mtaa Kilimanjaro na kina askari kumi na gari moja la kuzima moto ambalo kwa sasa lipo jijini Mbeya kwa ajili ya matengenezo,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa viti Maalum Swaumu Sakala (CUF) ameitaka serikali ieleze hatua zinazochukuliwa ili kuthibitii vifo vinavyotokana na utumiwaji wa bandari ya Pangani.

Mbunge huyo alisema bandari ya Pangani ni kati  ya bandari ambazo zinasababisha vifo vingi na visivyotangazwa. Chanzo cha vifo hivyo ikiwa ni ubovu wa vyombo vya usafiri vinavyotumiwa na bandari hiyo na uthibiti mdogo wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (Sumatra)

“Ni lini zitajengwa ofisi za Sumatra katika bandari hiyo ili kuondosha tabia yya vyombo vya usafirishaji kujaza mizigo kupita uwezo wa chombo husika na hatimaye kusababisha ajali?” alihoji Swaumu.

Hapo awali katika maelezo yake Swaumu alisema, “Kutokuwepo kwa ofisi ya SUMATRA katika bandari ya pangani kumesababisha watu kufa bila hata kutangazwa huku vyombo vya usafirishaji vikibeba abiria na mizigo mingi kupitiliza.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwini Ngonyani akijibu swali hilo amesema vyombo vyote vya usafirishaji vinatakiwa kufuata utaratibu uliopo japo ni kweli kwa sasa ajali nyingi za majini zinatokana na kutokuwepo kwa watumishi wa kutosha kutoka Sumatra.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!