Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Taratibu Watanzania nje ya nchi kupiga kura hazijakamilika
HabariHabari Mchanganyiko

Taratibu Watanzania nje ya nchi kupiga kura hazijakamilika

Sanduku la kura
Spread the love

SERIKALI imesema, bado inaangalia uwezekano kwa Watanzania waishio nje ya nchi, kupiga kura katika chaguzi mbalimbali zijazo. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 23 Mei 2019, bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati akijibu swali la Asha Abdul Juma, mbunge viti maalum (CCM)  aliyehoji, lini serikali itakamilisha utaratibu wa kuwezesha Watanzania wanaoishi nje kupata nafasi ya kupiga kura?

Akijibu swali hilo Waziri Majaliwa amesema, serikali inaendelea kuona kama utaratibu uliopo sasa unafaa kwa Watanzania hao kupiga kura.

Hata hivyo, amesema kabla ya kuruhusu raia hao kupiga kura, serikali itafuatilia mienendo ya Watanzania waishio nje ya nchi ikiwemo shughuli zao na kama bado wana uraia wa Tanzania au wameomba uraia wa nchi husika walizoko.

“Jambo hili ni la kisera, serikali imeendelea kuona utaratibu huo kama unaweza kufaa.  Sababu lazima tupate kujua nani yuko nje ya nchi, wanafanya shughuli gani na kama ni bado Watanzania au waliomba uraia wa nchi za nje.

“Na pindi sera hii itakapokamilika tutakapoona inafaa, tutakuja kujulisha Bunge na Watanzania pale inapofaa,” amesema Waziri Majaliwa.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!