Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yaadhimisha siku ya mtoto wa kiafrika kwa maboresho ya sheria
Habari Mchanganyiko

Tanzania yaadhimisha siku ya mtoto wa kiafrika kwa maboresho ya sheria

Ummy Mwalimu, Waziri wa TAMISEMI,
Spread the love

SERIKALI nchini Tanzania inatarajia kuazimisha siku ya mtoto wa Afrika kesho tarehe 16 Juni, 2020 huku ikimarisha mfumo wa kisheria kwenye ustawi wa watoto nchini, Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Maadhimisho hayo yanafanyika tarehe 16 Juni kila mwaka katika nchi za Afrika pamoja kuboresha ustawi wa mtoto.

Akizungumza na wanahabari, Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto amesema kuwa serikali ya Tanzania inaadhimisha siku hiyo kwa kuboresha mfumo wa upatikanaji wa haki ya mtoto. 

“Mifumo hiyo ni pamoja uendeshaji wa mashauri ya watoto waliokinzana na sheria, uendeshaji wa makao ya marekebisho ya mtoto waliopata hukumu, taratibu za kuwathiri mtoto, utoaji wa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya motto, utoaji wa ushahidi mahakamani na utekelezaji wa sheria ya mtoto namba 21ya mwaka 2009,” amesema Waziri Ummy.

Serikali inaendelea kutoa huduma za ustawi wa jamii kwenye mahabusu tano za watoto zilizopo Mbeya, Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Kilimanjaro.

Amesema kuwa mahabusu hizo zimelenga kutowachanganya watoto wenye kesi mahakamani na watu wazima.

Amesema serikali imeongeza mahakama ya kusikiliza mashauri ya watoto kutoka mahakama tatu mwaka 2015/2016 hadi kufikia mahakama 141 mwezi Machi 2020 lengo likiwa kuwa na mahakama ya watoto kwa kila wilaya nchini.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau tunatekeleza programu ya marekebisho ya tabia kwa watoto waliopatikana na makosa katika halmashauri mbalimbali nchini. Programu hiyo imefanya watoto waliopata huduma hiyo kuongezeka kutoka watoto 91 mwaka 2015/16 hadi watoto 501 mwezi Machi 2020.

Watoto wakiwa na furaha

Lengo la serikali ni kuwarekebisha watoto hao na kuwarejesha kwenye jamii wakiwa na tabia njema,” amesema Waziri Ummy.

Amesema kuwa Wizara kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameanzisha madawati maalamu ya watoto kwenye vituo 407 vya polisi.

“Tarehe 16 Juni siku ya mtoto wa Afrika chimbuko la maadhimisho hayo ni mauaji ya watoto takribani 2,000 yaliyofanywa na utawala wa Makaburu katika kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini tarehe 16 Juni, 1996. Mauaji hayo yalitokea wakati wa maandamano ya wanafanzi waliokuwa wakipinga mfumo wa elimu ya kibaguzi nchini Afrika Kusini,” amesema Waziri Ummy.

Mwaka 1991 viongozi wa umoja wa nchi za Afrika walifanya uamuzi wa kuienzi siku hiyo ikiwa ni kumbukumbu ya mauaji ya watoto hao.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali na wadau wengine wa ustawi wa mtoto hutumia siku hiyo kutathimini hali ya upatikanaji wa haki, ulinzi na usalama wa mtoto kwa lengo la kuboresha ustawi na maendeleo ya watoto.

Amesema kuwa kauli mbiu ya kuadhimisha siku ya mtoto mwaka huu ni ‘Mifumo rafiki ya upatikanaji wa haki ya mtoto ni msingi imara wa kulinda haki zao,’ iliyotoholewa kwenye kiengereza iliyokuwa ‘access to child freindly justice in Afrika.’

Amesema kuwa kauli mbiu hiyo itasaidia kuweka mifumo madhubuti na rafiki ya kushughulikia mashauri ya watoto.

Waziri Ummy amewasisitiza wazazi kuendelea kuchukua tahadhari kwa watoto juu ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu (Covid-19).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!