Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TADB Benki yatuhumiwa kupendelea wake wa vigogo
Habari Mchanganyiko

TADB Benki yatuhumiwa kupendelea wake wa vigogo

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Thomas Samkyi
Spread the love

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), imedaiwa kutoa mikopo kwa kupendelea zaidi wake wa vigogo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akiuliza swali bungeni leo tarehe 8 Mei 2019, Goodluck Mlinga, Mbunge wa Ulanga (CCM) amehoji, ni kwanini TADB inatoa mikopo kwa upendeleo hasa wake wa vigogo?

Akiuliza swali la nyongeza leo bungeni, Mlinga amedai kwamba, Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo kwa upendeleo kwa kuwaacha baadhi ya wanawake na kutoa kwa wake za vigogo.

Akijibu swali hilo Omari Mgumba, Naibu Waziri wa Kilimo ameeleza kuwa, tuhuma hizo si za kweli kwamba, wamekuwa wakipendelea kuwapa mikopo wake wa vigogo.

“Kwanza sio kweli, kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo tunatoa mikopo kwa upendeleo, benki hii tumeianzisha kwa lengo la kukuza uchumi.

“Tumewaelekeza wanawake wajiunge na vikundi na vikundi ndio vitakuwa dhamana, na tuliagiza asilimia 20 iende kwao na tumewaelekeza watoe mikopo kwa akina mama lakini benki hiyo imeishatoa asilimia 33 ya mikopo mpaka sasa,” amesema Mgumba.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum, Ester Mmasi (CCM) alitaka kauli ya serikali kuhusu ushiriki wa wanawake kwenye sekta ya kilimo.

“Changamoto kubwa inayowafanya wanawake wa Tanzania wasishiriki kwenye sekta ya kilimo ni ufinyu wa bajeti na mtaji kutoka taasisi za kifedha, Je, nini kauli ya serikali,? alihoji mbunge huyo.

Hata hivyo, Mgumba amesema sekta ya kilimo inajumuisha sekta ya ndogo ya kilimo mazao, mifugo, uvuvi na misitu.

“Bajeti ya Wizara ya Sekta ya kilimo zinajumuisha bajetiza wizara za sekta husika.Katika kutatua changamoto hizo.

Serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004,” amesema Mgumba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!