Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Siri zavuja mgogoro Lipumba Vs Maalim Seif?
Habari za SiasaTangulizi

Siri zavuja mgogoro Lipumba Vs Maalim Seif?

Spread the love

MIKAKATI inayofanywa na Kambi ya Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anayetambiliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ina lengo moja kuu. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Lengo linalotajwa ni kuhakikisha Maalim Seifa Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF anasambaratishwa kwa kuwa ni ‘kikwazo’ kwa maisha ya Prof. Lipumba ndani ya chama hicho na uimara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar.

Tarifa za ndani ya CCM na Serikali bara na visiwani zinasisitiza kuwa, Prof. Lipumba anasidiwa ili kuhakikisha anammaliza Maalim Seif.

“Mbona harakati za kumsaidia zipo wazi! Wewe angalia tu walivyokuwa wakihaha kufungua akaunti ili fedha za ruzuku ziingizwe, yale ni maelekezo,” kimeeleza chanzo kimoja ndani ya CCM Zanzibar.

Taarifa zaidi zinaeleza, harakati zote zinalenga kummaliza Maalim Seif ili Zanzibar ipumue baada ya kiongozi huyo kuwa mwiba usiopoa visiwani humo.

Amesema, mbinu kadhaa zimetumika na tayari zimefeli, ikiwa pamoja na kupenyezewa ruzuku, kuundwa bodi ya Lipumba hapo awali pia kutambuliwa na serikali.

Wakati Kambi ya Prof. Lipumba ikipenyeza majina kwa Wakala wa Usajili na Udhamini (Rita) kuunda Bodi ya Wadhamini CUF ili kuendelea kupata fedha za kuendesha vikao na shughuli ya kambi hiyo, mpango mwingine tayari umesukwa.

Mpango huo ni kuitisha mkutano mkuu ili kujaribu kumtimua Maalim Seif. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 12-15 Machi 2019.

“Maalim Seif anasukiwa mipango bara na visiwani. Muda wote wanajaribu kumwangamiza lakini wanashindwa.

“Harakati za kummaliza zilianzia visiwani zikafeli, sasa wanajaribu kupitia mgogoro wake na Lipumba.

“Sio kwamba Maalim Seif hajui, anapata taarifa zote na namna mambo yanasukwa. Wapo wanaompeyenzea taarifa hizi ingawa sijui mwisho wake ni nini?,” ameeleza mtoa taarifa huyo.

Amesema kuwa, mgogoro wa CUF una uhusiano mkubwa na ‘usumbufu’ wa Maalim Seif visiwani Zanzibar na kwamba, umesukumwa bara.

Kauli ya mtoa taarifa inashabihiana na ile iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu CUF Bara (Kambi Maalim Seif), Joran Bashange, katika ukumbi wa ofisi ya wabunge iliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Bashange alisema, Prof. Lipumba, anapanga kumwengua Maalim Seif kwenye Mkutano Mkuu huo.

Na kwamba, kambi hiyo ya Maalim Seif imetoa onyo kuhusu mkutano huo na kuwataka wajumbe kutohudhuria.

Kauli ya Bashange ilikwenda mbali zaidi na kueleza ‘tuko tayari kukilinda chama kwa gharama yoyote.”

Kwenye mkutano huo Bashange alidai, Prof. Lipumba anashirikiana na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, kupanga kumfukuza uanachama Maalim Seif na viongozi wenzake halali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!