Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Siri iliyojaa hofu CCM
Habari za Siasa

Siri iliyojaa hofu CCM

Spread the love

SAFARI ya kupeleka vilio ama vicheko kwa wateule wake waliopita kwenye kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inazidi kushika kasi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Tayari vikao vya kwanza vya kufyeka majina ya wateule ama kupitisha majina hayo kwenye ngazi ya Kamati za Siasa za Mikoa imefanyika.

Mpaka sasa, bado ni siri kwa kuwa haijulikani jina la nani limevuka kihunzi cha kwanza cha Kamati za Siasa za Wilaya. Vikao vinavyoendelea leo tarehe 4 Julai 2020, ni vya Kamati za Siasa za Mikoa baada ya kupokea majina na mapendekezo kutoka Kamati za Siasa za Wilaya.

Jina la nani limepitishwa kwenda kamati ya Siasa za Mikoa, ndio swali analojiuliza kila mgombea aliyepitishwa ama aliyeshindwa kwenye kura za maoni za chama hicho.

Mikutano mikuu ya CCM ya majimbo kwa ajili ya hatua ya awali ya kupendekeza wagombea ilifanyika Julai 20 hadi 21 2020, ikifuatiwa na vikao vya Kamati za Siasa za Wilaya vilivyofanyika tarehe 1 hadi 2 Agosti 2020.

Kwa mujibu wa Humprey Polepole, sasa wagombea ndio wanakwenda kupatikana na kwamba, wanaweza kuwa wale waliopitishwa kwenye kura za maoni ama la! Fumbo la nani amepitishwa kugombea bado halijateguliwa.

Kwa mujibu wa ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa Ubunge, Uwakilishi na Udiwani katika uchaguzi huo, wajumbe wa kamati hizo watatoa mapendekezo yao kuhusu wagombea katika Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) na Kamati Maalum ya NEC Zanzibar.

Kwa upande wa wagombea wa udiwani, tarehe 6 Agosti 2020 Vikao vya NEC ngazi ya mikoa vitafanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa udiwani wa kata na wadi pamoja na madiwani viti maalum.

Hata hivyo, vikao vya Baraza Kuu la Wazazi la CCM kupendekeza wabunge Viti Maalum kundi la wazazi vitafanyika tarehe 9 Agosti 2020, huku Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) litafanya kura za maoni kwa wagombea wa ubunge viti maalum tarehe 10 Agosti 2020.

Baada ya vikao hivyo kufanyika, mapendekezo yake yatawasilishwa katika vikao vya NEC.

CCM kilifungua zoezi la kutafuta wagombea wake katika uchaguzi huo tarehe 14 Julai mwaka huu, ambapo watia nia katika nafasi mbalimbali walianza kuchukua siku hiyo, na kisha kurejesha fomu hizo tarehe 17 Julai 2020.

Hadi sasa CCM kimeshapitisha wagombea Urais wa Tanzania na Zanzibar, ambapo Rais John Magufuli alipitishwa na Mkutano Mkuu wa chama hicho kugombea Urais wa Tanzania huku Dk. Hussein Mwinyi akipitishwa kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar.

Hali kadhalika, CCM imeshakamilisha kura za maoni kwa wagombea ubunge na uwakilishi, ambapo vinasubiriwa vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa (NEC), kwa Tanzania bara na Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, vitapitisha rasmi wagombea wa nafasi hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!