September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msajili avitaka vyama vya siasa kuzingatia sheria

Msajili msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahonza

Spread the love

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tazania, umetoa wito kwa vyama vya siasa nchini humo kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Msajili msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahonza mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) unaofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Nyahoza amekutana na kauli za wajumbe zilizokuwa zikikatisha hotuba yake.

“Nimehudhuria mkutano huu mara kadhaa na nipo hapa kumwakilisha msajili wa vyama na sisi tunakuja hapa kutekeleza wajibu wetu wa kisheria wa vyama vyote,” amesema Nyahoza huku sauti zikisikika zikisema ‘mbona msajili mwenyewe hatumwoni’

Akiendelea, Nyahoza amesema “ili kuhakikisha mikutano yenu inafanyika kwa kuzingatia sheria na kanuni. Kwenye haki kuna wajibu ikiwemo kusimamia sheria za nchi.”

Kisha sauti zikasikika zikisema ‘mbona kuna sheria mbovu.’

“Mwenyekiti (Freeman Mbowe), moja wapo ya misingi muhimu ya chama cha siasa, kama mnavyosema mnatetea demokrasia, msingi muhimu ni demokrasia ndani ya chama na demokrasia ni sehemu ya watu kuheshimu sheria.”

Akihitimisha hotuba yake, Nyahoza amesema “wito wetu kama ofisi ya msajili na mlezi, ninyi na vyama vyote mheshimu sheria na tunashauri tuheshimu sheria, tufanye uchaguzi kwa uhuru, haki na amani.”

error: Content is protected !!