Wamama wa kiislamu wakishiriki mchezo wa mbio za magunia

Sikukuu ya Eid yasherekewa kivingine Pugu

VIJANA mbalimbali wa dini ya Kiislamu wamefanya michezo katika viwanja vya Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaam ili kuwasaidia kutojiingiza katika maovu inapofika siku za sikukuu, anaandika Faki Sosi.

Tamasha hilo la michezo ambalo liliwashirikisha vijana lilifanyika jana katika sherehe ya sikukuu ya Eid El Hajj, linalenga kuwaweka pamoja na hivyo kuwafanya wasiende disco na sehemu zingine za starehe.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Kiislam, Yusuf Aboud ‘Babu Jongo’, amesema michezo iliyofanyika kwenye tamasha hilo ni pamoja na kukimbia kwa gunia, kukimbia na chupa kichwani na kuvuta kamba.

Aboud amewataka vijana wengi kujitokeza na kujiunga na Jumuiya hiyo kwa kuna mambo mengine wanaweza kufaidika nayo na siyo kuishia kufanya michezo pekee.

Jumuiya hiyo imefanikiwa kuimarisha maadili na amani kwa jamii katika eneo la Pugu na hiyo ni mara ya pili kufanyika tamasha hilo.

VIJANA mbalimbali wa dini ya Kiislamu wamefanya michezo katika viwanja vya Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaam ili kuwasaidia kutojiingiza katika maovu inapofika siku za sikukuu, anaandika Faki Sosi. Tamasha hilo la michezo ambalo liliwashirikisha vijana lilifanyika jana katika sherehe ya sikukuu ya Eid El Hajj, linalenga kuwaweka pamoja na hivyo kuwafanya wasiende disco na sehemu zingine za starehe. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Kiislam, Yusuf Aboud 'Babu Jongo', amesema michezo iliyofanyika kwenye tamasha hilo ni pamoja na kukimbia kwa gunia, kukimbia na chupa kichwani na kuvuta kamba. Aboud amewataka vijana wengi kujitokeza na kujiunga na Jumuiya hiyo kwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube