January 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yataka majibu ya corona kwa saa 24

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imeagiza utoaji wa majibu ya vipimo vya ugonjwa wa corona ndani ya saa 24 badala ya saa 72. Anaandika Regina Mkonde…(endelea).

Akizungumza na Uongozi wa Maabara ya Taifa na Afya ya Jamii, Prof. Abel Makubi ambaye ni Mganga Mkuu wa Serikali leo tare he 26 Desemba 2020 amesema, hatua hiyo itaondoa malalamiko ya ucheleweshwaji kwa wale wanaotaka kusafiri.

Prof. Makubi amekutana na uongozi wa maabara hiyo, wasimamizi wa maabara na waganga wakuu kutoka hospitali za serikali na binafsi.

Ni baada ya kufanya ziara katika maabara hiyo kwa lengo la kusikiliza na kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazokabili maabara hiyo.

“Ucheleweshaji wa majibu kamwe hauwezi kuvumiliwa,” amesema Prof. Makubi huku akisisitiza kuwepo malalamiko hayo hasa kutoka kwa wasafiri.

Ameutaka uongozi wa maabara hiyo kufanya lolote linalowezekana kuhakikisha wanatimiza la kutoa majibu ya vipimo vya corona ndani ya saa 24.

error: Content is protected !!