Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Safari hii sikubali – Maalim Seif
Habari za Siasa

Safari hii sikubali – Maalim Seif

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, hatokubali kuporwa ushindi endapo atashinda kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 27 na 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Ametoa kauli hiyo mbele ya wanachama wa chama hicho jana Jumapili tarehe 30 Agosti 2020, muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Maalim Seif ambaye anagombea urais visiwani humo kwa mara ya sita mfululizo, amedai mara zote alizogombea uchaguzi amekuwa akiporwa ushindi wake.

“Nasubiri ZEC initeue kisha ndio nitaongea. Safari hii sintokubali,” alisema Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho mbele ya wanachama wa chama hicho Vuga, Zanzibar.

Akizungumzia mahubiri ya amani yanayotolewa na viongozi mbalimbali wa dini nchini, Maalim Seif aliwakumbusha viongozi hao kuhubiri amani na haki.

“Bila haki hakuna amani,” alisema na kuongeza kuwa, haki ndio zao la amani na kwamba, kwenye uchaguzi huu, anataka uhuru na haki vitendeke.

Akizungumzia wagombea wa CCM kupita bila kupingwa, Maalim Seif ameeleza kwamba, ni hofu ya chama tawala dhidi ya wagombea wa vyama vya upinzani.

“Inaonesha wazi kwamba CCM wanaogopa uchaguzi, hawawezi kupambana kwa hoja. Tupo tayari kushindana,” alisema Maalim Seif.

Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo, amekuwa mgombea wa 12 kati ya 13 ambao tayari wamechukua fomu ya kugombea urais visiwani humo.

Wagomba ambao tayari wamechukua fumu visiwani humo ni pamoja na Dk. Hussein Mwinyi kupitia CCM, Said Soud (AAFP), Juma Ali Khatib (Ada Tadea), Hamad Rashid (ADC), Mfaume Khamis (NLD), Ali Juma (Chauma), Issa Muhammed Zonga (SAU), Ameri Said Ameri (Demokrasia Makini) na Hamad Muhammed Ibrahim (UPDP).

Wengine ni Shafii Hassan Suleiman (Democratic Party), Khamis Faki Mgau (NRA), Maalim Seif Sharif Hamad (ACT- Wazalendo) na Othman Rashid Khamis (CCK).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!