Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Magufuli, Alhaj Mwinyi, Makinda wamuaga Dk. Mengi
Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Magufuli, Alhaj Mwinyi, Makinda wamuaga Dk. Mengi

Spread the love

RAIS John Magufuli ameongoza mamia ya Watanzania ikiwemo viongozi wa serikali, wanasiasa na wafanyabiashara kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni zilizo chini ya IPP Group, Dk. Reginald Mengi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mwili wa Dk. Mengi umeagwa leo tarehe 7 Mei 2019 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Dk. Mengi alifariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 2 Mei 2019.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika ibada ya kuuaga mwili wa Dk. Mengi ni pamoja na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

 Pia walikuwepo viongozi wastaafu akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Al Haji Hassan Mwinyi; Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mizengo Pinda; Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela na Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda.

Wanasiasa walioshiriki ibada ya kuuaga mwili wa Dk. Mengi ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na wasanii mbalimbali.

Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Rais John Magufuli, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema, serikali imepata pigo kwa kuondokewa na mtu muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Prof. Kabudi amesema, serikali inatambua mchango Mkubwa wa Dk. Mengi alioutoa akiwa hai ikiwemo katika kushiriki shughili za ukuzaji uchumi, uhifadhi wa mazingira na kusaidia wenye uhitaji ikiwemo walemavu.

“Serikali imehudhunishwa sana na kifo cha Dk. Mengu, nchi imeondokewa na mtu mnyenyekevu na mwenye upendo. Alishiriki katika utunzaji wa mazingira, Dk. Mengi alifanya mengi ya kujifunza,” amesema Prof. Kabudi na kuongeza;

“Serikali inatambua mchango mkubwa Dk. Mengi alioutoa kwa jamii, tunatambua mchango wake kwa Watanzania wote masikini, walemavu na wenye uhitaji, mchango wake kwa jamii ulifanya atambulike na kupata tuzo mbalimbali za kimataifa.”

Prof. Kabudi amesema, kabla ya umauti kumfika Dk. Mengi alipanga kuanzisha viwanda ikiwemo cha uundaji magari na dawa kwa kushirikiana na wawekezaji wa nje.

Pia, Prof. Kabudi amesema, Dk. Mengi alikuwa kipaumbele katika kuishawishi serikali kuwaamini pamoja na kuwapa fursa za uwekezaji wazawa.

“Serikali imeguswa sana na kifo cha Dk. Mengi katika uhai wake amefanya mengi ikiwemo kushiriki katika uchumi kwa uwekezaji wake na kushiriki moja kwa moja katika ukuzaji uchumi na kutoa ajira, hakusita kusaidia wawekezaji wazawa kuwekeza nchini,

alishauri serikali kushirikisha wazawa katika uwekezaji. Kwa serikali ya awamu ya tano, Dk. Mengi alikuwa mzawa na mzalendo mkweli katika kufanikisha sera ya viwanda na kufikisha uchumi wa kati.” Amesema Prof. Kabudi.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kifo cha Dk. Mengi kimeacha pigo kubwa kwa Wanatasnia ya michezo na habari, kutokana na mchango wake mkubwa aliokuwa anautoa katika tasnia hizo.

“Huwezi kuiongelea sekta ya habari Tanzania bila kugusia mchango mkubwa wa marehemu, alianzisha magazeti, televisheni na redio. Amefariki akiwa Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), huwezi kuongelea sanaa nchini bila kumgusa marehemu Dk. Mengi kutokana na kazi za sanaa kupata sehemu ya kurushwa,” amesema Dk. Mwakyembe na kuongeza;

“Kila sehemu wameguswa, Ndugu Mengi maeondoka na amemgusa kila Mtanzania, na mimi naweza kuelewa kwa nini kila mtu ameguswa. Aliamini katika taifa na aliamini katika utaifa na maendeleo ya kila mtanzania lakini maendeleo hayo yapatikane katika nchi yenye amani na upendo.”

Akitoa salamu za familia, Balozi Juma Mwapachu amesema, marehemu Dk. Mengi enzi za uhai wake hakujihusisha na siasa, lakini alikuwa na maono ya kisiasa yalisaidia kuimarisha mahusiano kati ya serikali na sekta binafsi.

“Mengi hakujihusisha na siasa, lakini haimaanishi hakuwa na maono ya kisiasa, aliamini kwake kufanikiwa kunategemea kuwepo kwa imani na kufanikiwa na mahusiano kati ya serikali na sekta binafsi,” amesema Balozi Mwapachu na kuongeza.

“Katika kitabu chake alionesha namna alivyopata mafanikio katika biashara zake na kusaidia jamii, kila wakati marehemu Rodney alimtaka baba yake aandike kitabu cha kuhusu maisha yake, rais alimtaka mengi atafsiro kiswahili. Leo sio siku ya kuongea mengi kuhusu imani ns mafanikio ya mengi, ameacha mafanikio makubwa kwa nchi yetu.”

Balozi Mwapachu ameishukuru Serikali na watanzania kwa ujumla kwa niaba ya familia ya marehemu Dk. Mengi kwa kujitoa kwake katika kufanikisha usafirishaji wa mwili wa mfanyabiashara kutoka mjini Dubai alikofariki dunia hadi kufika hapa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!