Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Profesa Lipumba: CUF hatutashiriki uchaguzi tena
Habari za Siasa

Profesa Lipumba: CUF hatutashiriki uchaguzi tena

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

CHAMA Cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania, kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wowote ujao hadi mazingira ya uchaguzi huru na wa haki yatakapopatika ikiwemo Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Msimamo huo umetolewa leo Jumatatu tarehe 2 Novemba 2020 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba alipokuwa akitoa tathimini ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Uchaguzi huo, CUF kimepata mbunge mmoja, Shamsia Mtamba wa Mtwara Vijijini aliyemwangusha Hawa Ghasia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku Profesa Lipumba mwenyewe aliyegombea urais alipata kura 72,885 kati ya milioni 15 waliopiga kura.

Dk. John Pombe Magufuli alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata kura milioni 12.5 kati ya kura 15 milioni zilizopigwa. Waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura walikuwa milioni 29.7.

Profesa Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari amesema, uamuzi huo unatokana na chama hicho kutoridhishwa na mchakato wa uchaguzi uliopita, kuanzia upigaji kura hadi kutangazwa kwa matokeo yake.

“Hatukubaliani na matokeo kwa sababu tumeibiwa sana, mfano Jimbo la Temeke mgombea wetu wa Ubunge katika kituo alichopiga kura yeye na familia yake amepata kura sifuri ina maana hata mwenyewe hakujichagua,” amehoji Profesa Lipumba.

Mwenyekiti huyo wa CUF amesema, chama hicho hakitashiriki uchaguzi wowote, badala yake kitajikita katika harakati za kudai katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Hata hivyo, Profesa Lipumba amewaomba Watanzania kufanya maombi ya kitaifa ili kumuomba Mungu atoe haki juu ya makosa yaliyofanyika katika uchaguzi huo.

“Tunawaomba Watanzania wote wapenda haki kuungana na sisi katika ibaada siku ya Alhamisi, ambapo tutafunga kwa kutokula mchana na tufanye dua na maombi kila mmoja kwa imani yake ili kuomba hukumu ya haki kutokana na kile kilichofanyika,” amesema Prof. Lipumba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!