Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nondo: Mahakama iwape dhamana viongozi Bavicha
Habari za Siasa

Nondo: Mahakama iwape dhamana viongozi Bavicha

Spread the love

NGOME ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo kimelaani viongozi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), kunyimwa dhamana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Viongozi walionyimwa dhamana ni Nusrat Hanje, Katibu Mkuu wa Bavicha, Twaha Mwaipaya, Mratibu wa Uhamasishaji wa baraza hilo, Samwel Gishinde Malo, Katibu wa Chadema Singida na wengine watano.

Tamko hilo limetolewa leo Jumamosi tarehe 1 Agosti 2020 na Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo jijini Dar es Salaam, ikiwa zimepita siku 26 tangu viongozi hao wakamatwe na Jeshi la Polisi mkoani Singida tarehe 6 Julai 2020.

Hanje na wenzake wanakabiliwa na kesi ya Jinai Na. 115/2020 katika Makahama ya Mkoa wa Singida, ambapo wanatuhumiwa kufanya makosa manne ikiwemo mkusanyiko usio halali, kudharau bendera na wimbo wa Taifa, vitendo vinavyohatarisha amani.

Akizungumzia sakata hilo, Nondo ameitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kuwapa dhamana viongozi hao kwa kuwa makosa wanayotuhumiwa yana dhamana.

“Takribani ni mwezi sasa vijana wenzetu ambao ni viongozi wa kitaifa Bavicha, Hanje, Mwaipaya na viongozi wengine bado wameshikiliwa na kunyimwa dhamana kwa makosa yenye dhamana. Tujiulize Katibu Nusrat na wenzake kipi wamefanya kuhatarisha maslahi au usalama wa Jamhuri,” amehoji Nondo.

Baada ya viongozi hao wa Bavicha kunyimwa dhamana na Mahakama ya Mkoa wa Singida, yalikatiwa rufaa katika Mahakama Kuu Dodoma, ambapo kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa Jumatatu tarehe 3 Agosti 2020.

“Maamuzi hayo ya mahakama ya Singida yalikatiwa rufaa katika mahakama kuu Dodoma na Jumatatu tarehe 3 Augosti tunajua kesi inaenda kusikilizwa. Hivyo, tunaomba mahakama kuu ya Dodoma kutenda haki kwa vijana wetu hawa, ” amesema Nondo.

Nondo amesema, Hanje na wenzake kunyimwa dhamana katika kipindi hiki cha uchaguzi ni kuwanyima haki yao kikatiba kwa kuwa wanagombea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020.

“Tunaiomba mahakama itende haki kwa kuzingatia pia vijana hawa ni wagombea katika maeneo tofauti tofauti nchini, hivyo kuwanyima dhamana bila sababu za msingi katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu, ni kuvunja haki yao ya kikatiba ya kugombea kinyume na ibara ya 21(1) na 67(1) ya katiba yetu ya nchi,” amesema Nondo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!