Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NBS yaeleza hali ya umasikini nchini
Habari Mchanganyiko

NBS yaeleza hali ya umasikini nchini

Dk. Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Spread the love

DAKTARI Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), amesema kasi ya upunguaji umasikini kwa Watanzania imeongezeka, ukilinganisha na nchi za Afrika. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Chuwa ametoa kauli hiyo leo tarehe 17 Februari 2020, jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathimini ya hali ya umasikini wa kipato cha kaya binafsi nchini, katika uzinduzi wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF.

Dk. Chuwa amesema, kwa mujibu wa tafiti  za mapato na matumizi ya kaya binafsi, zilizofanywa na Ofisi ya Takwimu kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia (WB), umasikini umepungua kutoka asilimia 39 mwaka 1991/92 hadi kufikia asilimia 26.4 mwaka 2018.

Dk. Chuwa amesema, utafiti huo hufanyika kila baada ya miaka mitano, ambapo utafiti huo huchunguza mapato na matumizi ya kaya katika kipindi cha miezi 12.

“Hali ya umasikini inapimwa na utafiti ujulikanayo na mapato na matumizi ya kaya binafsi, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, tunachukua taarifa za wanafamilia wa kaya binafsi, juu ya mapato yao na matumizi yao kwa miezi 12, zimeendelea kufanyika hata wakati wa mkoloni, na zilianza kufanyika mwaka 1991,” amesema Dk. Chuwa na kuongeza:

“Hali ilkuwaje?, mwaka 1991/92 umasikini wa kipato ulikuwa asilimia 39 asilimia, 2007 umasikini ulikuwa asilimia 34, 2012 asilimia 28.4, 2018 ambao tunafanya na kila baada ya miaka mitano, ulikuwa asilimia 26.4. Hivyo, kasi ya umasikini kupungua inaongezeka kwa kasi.”

Dk. Chuw amesema Tanzania umasikini wake unapungua kwa kasi na kuzishinda nchi kadhaa barani Afrika, ikiwemo Kenya ambayo hali ya umasikini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2015, ulikuwa asilimia 36.3. Afrika Kusini asilimia 55.5, Zambia asilimia 54.4.

“Hii ndio hali ya umasikini kwa mahitaji ya msingi kwa baadhi ya nchi za Afrika, tuangalie Tanzania tulipo, hatua tuliyoipiga. Katika utafiti huu huwa tunakokotoa viashiria vya huduma ya jamii, inathibitisha nchi yetu imepiga hatua kubwa, nasema kwa kuwa utafiti huu ulitupiwa macho mara 6 na uliangaliwa na WB na UN,” ameeleza Dk. Chuwa.

Dk. Chuwa amesema, viashiria vinavyothibitisha hali ya umasikini nchini inapungua kwa kasi ni, upatikanaji wa huduma bora ya maji, elimu na makazi bora ya wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!