September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kabendera atakuwa huru kesho?

Spread the love

HATMA ya Mazungumzo kati ya Erick Kabendera na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kufahamika jumatatu tarehe 17 Februari 2020. Anaandika Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Awali tarehe 11 Februri 2020, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilielezwa na Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi kuwa  Upande huo unaomba kuzungumza na mshtakiwa mwenyewe juu ya kukiri makosa yake.

Wakili Nchimbi aliieleza Mahakama hiyo kuwa upande wa Mashtaka na ule wa utetezi upo kwenye majadiliano ya kukiri kwa muda mrefu sasa na yanafikia mwishoni.

Nchimbi ameiomba mahakama hiyo kuaharisha shauri hilo mpaka tarehe 17 Februari mwaka huu .

Wakili wa Utetezi Jebra Kambole alikubaliana na maombi  haya na kuieleza mahakama hiyo kuwa upande huu haupingi jamhuri kuzungumza na mtuhumiwa huyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Janneth Mtega aliruhusu mazungumzo hayo na kuahirisha shauri hilo mpaka tarehe 17 Februari 2020.

Mazungumzo hayo yapo kisheria kifungu cha  3 na kuongeza kifungu cha 194 A 194 H cha sheria ya Makosa ya jinai ya mwaka 1985 sura ya 20 (Plea Bargaining), ambapo mtuhumiwa anapewa nafasi ya kukiri na kuiomba msamaha na baadaye kuachiwa huru.

Hivyo huenda Kabendera akaachiwa huru Jumatatu ya kesho kutokana na zao la mazungumzo hayo.

Kabendera anashitakiwa kwenye mahakama hiyo kama makosa matatu ikiwamo mshtakiwa anadaiwa katika siku tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 jijini Dar es Salaam, alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Katika shtaka la pili, inadaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa bila kuwa na sababu za msingi kisheria alishindwa kulipa kodi ya Sh173.24 milioni ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la utakatishaji fedha,  kati ya Januari 2015 na Julai 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia kiasi hicho cha Sh173.2 milioni wakati akizipokea alijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kukwepa kodi na kujihusisha na genge la uhalifu.

error: Content is protected !!