Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM amgeuka Makonda,amtaka arejeshe fedha za TASAF
Habari za Siasa

JPM amgeuka Makonda,amtaka arejeshe fedha za TASAF

Spread the love

FEDHA za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), alizotumbua Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2012, ametakiwa kuzirejesha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Agizo hilo limetolewa na Rais John Magufuli, leo tarehe 17 Februari 2020, wakati akizindua kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya Tasaf, jijini Dar es Salaam.

Awali, Makonda alieleza kwamba amenufaika na fedha za mfuko huo na kuwa, mwaka 2012 alipewa fedha za Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kwenda Dodoma kugombea umakamu mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

“Namshukuru sana Mzee Mkapa kuona bado anaendelea kufanya kazi yake, naomba Rais Magufuli niseme mbele yako mfuko huu wa Tasaf nami nimenufaika nao, haikuwa moja kwa moja.

“Lakini wakati naomba nafasi ya  makamu mwenyekiti wa vijana (UVCCM), Mkapa ndio aliyenipa nauli ya kwenda kuomba kura Dodoma. Kwa hiyo naimani ilikuwa sehemu ya huu mfuko, alikuwa na moyo,” alisema Makonda.

Kutoka na kauli hiyo, Rais Magufuli wakati akifanya tathmini ya mradi huo katika kupitia kaya masikini mwaka 2017 amesema, kaya 22,030 walibainika kutokuwa masikini licha ya kutumia fedha za Tasaf.

“Kupitia zoezi la kaya masikini, Nemvemba 2015 hadi wezi Juni 2017 tuliweza kubaini uwepo wa kaya hewa 73561. Kaya 22,030 zilithibitika kuwa wana kaya wake sio masikini, na hapa nafikiri ni miongoni na wakina Makonda ambao walizitumia hizi fedha kwenda safari ya Dodoma wakati sio masikini.

“Na ninaomba, kama hili ndio ukweli, Makonda azirudishe hizi fedha, fedha za TASAF akaenda nazo huo aliokuwa anaeleza, inawezekana nimemsikia vibaya na yeye hahusiki kwenye kaya masikini, make muangalie, hizo fedha lazima azirudishe,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Kwa hiyo, ni kaya 22,034 zilikuwa zilithibitika kuwa, wana kaya wake sio masikini, inawezekana huyo wa 34 yule ndio Makonda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!