Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mlipuko wa bomu wauwa mmoja na kujeruhi wawili Kibaha
Habari Mchanganyiko

Mlipuko wa bomu wauwa mmoja na kujeruhi wawili Kibaha

Spread the love

MBARAKA Koromera (37) amepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa katika mlipuko wa kifaa kinachodhaniwa kuwa bomu, uliotokea maeneo ya Msangani wilayani Kibaha mkoa wa Pwani. Anaripoti Hamisi Mguta…(endelea).

ACP Wankyo Nyigesa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani amesema tukio hilo limetokea jana tarehe 20 Septemba 2019, majira ya saa tano asubuhi.

Kamanda Nyigesa ameeleza kuwa, mlipuko huo umetokea wakati marehemu Koromera anachambua vyuma chakavu kwenye pagale la mtu aliyefahamika kwa jina la Rajab Nyangale.

Kamanda Nyigesa amewataja waliojeruhiwa kwenye mkasa huo kuwa ni, Fatuma Likupila na Shomari Athumani ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Tumbi wilayani Kibaha.

Amesema baada ya tukio hilo kutokea, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilifika eneo la tukio na kukuta vipande vitano vidhaniwazo kwamba ni mabomu, ambavyo inafanyia upelelezi.

“Katika eneo la tukio ambako Jeshi la Polisi tulifika kwa kusaidiana na JWTZ tumeokota vipande 5 vidhaniwavyo kuwa ni mabomu kwa ajili ya uchunguzi,” amesema Kamanda Nyigesa.

Kamanda Nyigesa ametoa tahadhari kwa wananchi kutohifadhi vyuma chakavu ndani ya nyumba pamoja na kutookota ovyo vifaa chakavu.

“Tunatoa rai kwa wananchi kuwa waangalifu, kuhifadhi vyuma chakavu nje ya nyumba. Na vyuma chakafu visiokotwe bila ya kupata ushauri wa watalaamu,” amesema Kamanda Nyigesa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!