April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

IGP Sirro aonya Polisi kujihusisha na siasa

IGP Simon Sirro

Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka askari polisi kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, na kukwepa kujihusisha na masuala ya siasa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

IGP Sirro ametuma salamu hizo leo tarehe 21 Septemba 2019, wakati akizungumza na askari polisi jijini Arusha.

IGP Sirro ameeleza kuwa, Jeshi la Polisi haliko kwenye upande wa siasa, na kuwa askari polisi wanapaswa kusimamia sheria.

“Sisi tunasimamia sheria, sisi hatuko kwenye upande wa siasa. Kwa hiyo simamia sheria zilizopo. Wajibu wetu mkubwa ni kusimamia sheria, kwa hiyo salamu zangu ni hizo,” amesema IGP Sirro.

Aidha, IGP Sirro amewataka askari polisi nchini kuwa waadilifu huku akionya wenye tabia ya kuuzia wenzao sare za polisi, akisema kwamba hatowavumilia.

“Sikuteuliwa IGP kuja kufukuza askari, kwa askari asinilazimishe kumfukuza,” amesema IGP Sirro.

error: Content is protected !!