Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mgombea Ubunge CCM afariki dunia
Habari za SiasaTangulizi

Mgombea Ubunge CCM afariki dunia

Spread the love

SALIM Abdullah Turky (57), mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Mpendae, Unguja, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Turky ambaye afahamika kwa jina maarufu la Mr White, alikutwa na mauti usiku wa kuamkia leo, tarehe 15 Septemba, mjini Unguja.

Alikuwa mbunge wa Mpendaye aliyechaguliwa katika uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015 na kutumikia nafasi hiyo, hadi mauti yanamkuta. Katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu, Turky alipitishwa na chama chake, kugombea tena nafasi hiyo.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, amethibitisha kufariki dunia kwa mwanasiasa huyo mashuhuri Visiwani Zanzibar.

“…tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Ndg. Salim Abdullah Turky (Mr White), mgombea ubunge wa CCM, jimbo la Mpendae, Zanzibar,” ameeleza Polepole kupitia ukurasa wake wa twitter.

Akaongeza, “tunatoa salamu za pole kwa familia, wanaCCM, wadau wa sekta binafsi nchini na wote walioguswa na msiba huu….”

Salim Hassan Turky, aliyezaliwa 11 Februari 1963, mjini Unguja, anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo, kijijini kwake, Fumba, takribani umbali wa kilomita 65 kutoka jimboni kwake, Mpendae, wilaya ya Mjini Magharibi.

Wakati wa uhai wake, hasa alipokuwa bungeni, Turky alikuwa miongoni mwa wabunge wachache, waliojitambulisha kuwa wawakilishi wa wananchi, kwa kutoweka mbele itikadi za kisiasa.

Atakumbukwa na wengi kwa mchango wake mkubwa aliyoutoa wakati wa shambulio dhidi ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

Ni Turky aliyedhamini malipo ya ndege iliyomchukua Lissu kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dodoma hadi Nairobi, nchini Kenya.

Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi – Amin.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!