BEKI wa klabu ya Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amefungiwa michezo mitatu baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kiwiko mchezaji Andrew Simchimba kwenye mchezo dhidi Coastal Union uliochezwa 3 februari, 2019. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)
Mchezaji huyo ambae alihojiwa na kamati ya nidhamu hapo jana alikili kosa hilo na kusema haikuwa dhamila yake bali alikuwa akijaribu kumzuia asipite hivyo kamati ikaamua kumsimamisha michezo mitatu mfululizo.
Afisa Habari wa shirikisho la mpira Tanzania TFF Clifford Ndimbo ameeleza kuwa Kamati hiyo ambayo ilikutana jana jumapili chini ya mwenyekiti wake wakili Kiomoni Kibamba.
“Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza michezo mitatu mfululizo kwa mujibu wa kifungu cha 48(1) (d) cha kanuni ya nidhamu” alisema Ndimbo
Hapo awali mcherzaji huyo aliitwa na kamati ya nidhamu ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Tff na kushindwa kutokea kutokana na timu yake kuwa katika michezo mikoani.
Ninja ambae kwa sasa amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga ataikosa michezo dhidi ya Lipuli Fc, Ndanda na African Lyon.
Leave a comment