Njalu Daudi, Mbunge aliyemaliza muda wake wa Itilima Mkoa wa Simiyu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa na Hayati Benjami Mkapa

Mbunge akumbuka wema wa Mkapa

Spread the love

MBUNGE aliyemaliza muda wake wa Itilima Mkoa wa Simiyu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Njalu Daudi amesema, wananchi wa jimbo hilo watamkumbika Hayati Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamini William Mkapa kwa mchango wake kwenye sekta ya afya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu … (endelea).

Mkapa amefariki dunia Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa tatizo la mshituko wa moyo na mwili wake utazikwa Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Daudi ambaye ameongoza kura za maoni kutetea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, amesema Hayati Mkapa alikuwa mzalendo wa kweli kwa Taifa na Afrika.

Amsema enzi za uhai wa Mkapa aliyeongoza Tanzania kwa miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 aliwasaidia kujenga jengo la upasuaji kupitia Taasisi ya Mkapa Foundation katika kata ya Nkoma.

“Alikua ni rafiki yangu, taifa limepoteza shujaa wa nchi na nguzo ya Afrika, tumuombee apumzike kwa amani,” amesema Daudi.

“Aidha kwetu katika kata ya Nkoma, tulikua na tatizo la kutokua na chumba cha upasuaji, Mkapa alihakikisha kupitia Mkapa Foundation anatimiza ndoto za wananchi wengi waishio Nkoma.”

“Sasa wazazi na wananchi wanapata huduma zote vyema na katika sehemu salama, alitumia zaidi ya Sh.270 million na kwa kweli ameacha alama maishani mwetu,‘’ amesema Silanga

MBUNGE aliyemaliza muda wake wa Itilima Mkoa wa Simiyu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Njalu Daudi amesema, wananchi wa jimbo hilo watamkumbika Hayati Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamini William Mkapa kwa mchango wake kwenye sekta ya afya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu … (endelea). Mkapa amefariki dunia Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa tatizo la mshituko wa moyo na mwili wake utazikwa Jumatano tarehe 29 Julai 2020. Daudi ambaye ameongoza kura za maoni kutetea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, amesema Hayati Mkapa alikuwa mzalendo wa kweli kwa Taifa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!