September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Muuza matikiti ambwaga diwani aliyeongoza miaka 20

Paul Kabugwe, kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katikati

Spread the love

PAUL Kabugwe, kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameacha historia kwa kumbwaga katika kura za maoni Ibrahimu Kalunga, aliyekuwa diwani wa Kata ya Nyakaliro, Sengerema mkaoni Mwanza kwa miaka 20. Anaripoti Mwandishi Wetu, Sengerema … (endelea).

Kabugwe ni ni mjasilimali anayejishughulisha na uuzaji wa matikiti maji Kata ya Nyakaliro Wilayani Sengerema

Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo Masumbuko Bihemo amesema, Kabugwe amepata kura 87 ambapo Kalunga aliyekuwa akitetea nafasi yake akipata kura 40.

“Wagombea katika nafasi hiyo walikuwa wanane, wapiga kura walikuwa 138 na kura zilizoharibika zilikuwa nane. Wagembea wengine mmoja kapata kura tatu na mwingine 0,” ameeleza Bihemo.

Wilaya ya Sengerema ina juma ya Kata 47, hata hivyo ni kata 16 tu ndiyo waliokuwa madiwani wake wamefanikiwa kutetea nafasi zao.

error: Content is protected !!