WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene amepiga marufuku, makongamano ya dini au mikutano ya mikesha inayofanyikia viwanja vya wazi usiku wa kuamkia mwaka mpya ambayo ni leo alhamisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Makongamano na mikutano hiyo huwa inafanyika kila tarehe 31 Desemba kuuaga na kuukaribisha mwaka mpya na mwaka huu yalikuwa yafanyike viwanja mbalimbali ikiwemo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, jana Jumatano tarehe 30 Desemba 2020, Waziri Simbachawene alizuia mikutano na makongamano hayo nchi nzima ambayo yangefanyika leo na kuagiza yafanyikie kanisani na mwisho iwe saa 6:30 usiku huku akionya watakaokaidi agizo hilo, watachukuliwa hatua.
Taarifa yote ya Waziri Simbachawene hii hapa;
Leave a comment