Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Malinzi aburuzwa mahakamani, wapo pia vigogo wa Simba
MichezoTangulizi

Malinzi aburuzwa mahakamani, wapo pia vigogo wa Simba

Kutoka Kushoto ni Selestine Mwesigwe, Katibu Mkuu wa TFF, Jamal Malinzi, Rais wa TFF, Geofrey Kaburu Makamu wa Rais wa Simba na wa mwisho Evance Aveva Rais wa Simba, wakiwa mahakamani Kisutu
Spread the love

JAMAL Malinzi (57), Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), anatarajiwa kufikishwa mahakamani mchana huu jijini Dar es Salaam, kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, anaandika Shafiyu Kyagulani.

Taarifa kutoka ndani ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) zinasema, Malinzi anafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako anatarajiwa kukabiliwa na mashitaka kadhaa ya ufujaji wa fedha za shirikisho, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Mbali na Malinzi wengine wanaofikishwa mahakamani pamoja naye, ni katibu mkuu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa, Rais wa Simba, Evance Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu.

“Ndio. Rais wa TFF na katibu mkuu wake, wote wawili tunawashikilia na watafikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma zinazowakabili,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa Takukuru ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini.

Alipoulizwa kipi hasa kilichoisukuma Takukuru kuwakamata na hatimaye kutaka kuwafikisha mahakamani Malinzi na Mwesigwa, kiongozi huyo alisema, “…hayo mengine yatafahamika mahakamani. Mimi siyo msemaji wa Takukuru.”

Amesema, “ulinichoniuliza, ndicho nilichokujibu. Kama kuna una mengine, mtafute mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Mlowola (Valentino Longino Mlowola). Yeye ndiye anayeweza kukueleza kwa kirefu ambacho kinawapeleka watuhumiwa mahakamani.”

Huku Malinzi na Mwesigwa wakipelekwa mahakamani, ndani ya TFF mchana huu wa leo –tarehe 29 Juni 2017 – kumepangwa kufanyika usaili kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.

Miongoni mwa nafasi hizo, ni rais wa shirikisho hilo, makamu wa rais na wajumbe wa kamati tendaji. Malinzi ni miongoni mwa wanachama wa TFF waliomba kugombea urais.

Malinzi amekuwa anatuhumiwa na wanachama wenzake wa shirikisho hilo kuendesha shirika hilo la umma kama kampuni yake binafsi. Anadaiwa kutenda upendeleo katika kutoa nafasi za uongozi; na au ajira kwa watu wanaotoka katika mkoa wake wa Kagera.

Miongoni mwa wanaotajwa, ni pamoja na katibu mkuu Mwesigwa; Evodius Mtawala, aliyekuwa mkurugenzi wa vyama wanachama na masuala ya kisheria wa TFF na “wakili msomi” – Julius Lugaziya, mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya uchaguzi ya shirikisho hilo.

JAMAL Emilly Malinzi, alizaliwa mjini Bukoba, mkoani Kagera, mwaka 1960.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!