Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kadinali ashtakiwa kuwanyanyasa watoto kingono
Kimataifa

Kadinali ashtakiwa kuwanyanyasa watoto kingono

Meza ya Hakimu
Spread the love

George Pell, Kadinali wa kanisa katholiki ameshitakiwa na Polisi nchini Australia kwa makosa kadhaa ya kuwanyanyasa watoto kingono, anaandika Hamis Mguta.

Kadinali huyo mwenye ushawishi mkubwa nchini humo amekanusha makosa hayo ambayo yanasemekana kufanyika miaka ya 1970 na anatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya Melbourne mwezi Julai.

Hata hivyo, wakilishi wa kanisa hilo hawajatoa tamko lolote juu ya swala hilo licha ya Shirika la BBC kutoa ombi ya kuwataka kufanya hivyo.

Idara ya Polisi iliamua kuchukua hatua ya kumfungulia mashtaka Kadinali Pell, baada ya kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa mashtaka mwezi uliyopita.

Naibu kamishna wa polisi amesema mchakato wa kumfungulia mashtaka kadinali huyo, hauna tofauti  na uchunguzi wowote.

Kadinali Pell ambaye anashitakiwa kutokana na madai ya “kihistoria” ni mweka hazina wa Vatican na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini Australia

Kadinali George Pell akiwa Vatican

“Madai hayo yalitolewa na zaidi ya mtu mmoja” amesema Naibu Kamishna wa Polisi Shane Patton.

Akiwa mweka hazina wa Vatican kadinali Pell anatambulika kuwa Afisa wa tatu mkuu katika kanisa katoliki na kuwa yuko tayari kufika mahakamani na atatetea mashtaka yanayomkabili.

“Kadinali Pell atarudi nchini Australia kwa haraka iwezekanavyo ili kujisafishia jina lake kufuatia ushauri ulioungwa mkono na madktari wake ambao pia watamshauri kuhusu mipango yake ya kusafiri” kanisa hilo lilieleza katika taarifa yake.

Kadinali huyo sio mkuu wa kanisa katoliki nchini Australia bali pia ni miongoni mwa viongozi wakuu walio na hadhi ya juu katika ulimwengu wa kanisa hilo.

Katika kipindi cha miongo miwili amekuwa amekuwa katika mstari wa mbele katika mjadala wa kanisa hilo kuhusu maswala tata kama vile lile la wapenzi wa jinsia moija ,ukimwi na utafiti wa seli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!