August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Mwinyi anatupeleka pabaya’

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ateta jambo na Rais Magufuli

Spread the love

WAZEE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamemtaka John Magufuli, Rais wa Tanzania kujitokeza na kutoa msimamo wake kuhusu kauli ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi iliyoshawishi Rais Magufuli awe Rais wa siku zote, anaandika Mwandishi wetu

Hayo yameelezwa na Roderick Lutembeka, Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee Chadema Taifa baada ya Rais Mstaafu Mwinyi kutoa kauli hiyo akiwa katika ibada ya Eid El Fitr kwenye viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam.

“Kama si matakwa ya Katiba ya nchi, uongozi wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwapo miaka yote..laiti ingelikuwa Katiba iliyopo haikufupisha muda wa uongozi wa rais, ningeshauri Rais Dk. Magufuli awe Rais wa Tanzania wa siku zote,” alisema Mwinyi katika ibada hiyo.

Unaweza kutazama video hapo chini kujua zaidi…

https://youtu.be/6ClEItLwGF8

Lutembela amesema, Rais huyo Mstaafu anaendeleza kiu ya kutaka kuondoa ukomo wa muda wa kutawala kwa Rais aliyokuwa nayo tangu 1992 pamoja na kukemewa na Mwal. Nyerere.

“Tulijipa muda tukiamini kuwa aliteleza ulimi na angeweza kurekebisha kauli yake lakini hakufanya hivyo…mbaya zaidi Rais mwenyewe naye amenyamaza kimya. Tukajua wazi kuwa huu ni mkakati rasmi wa kuliandaa taifa kisaikolojia kuwa na “Mfalme na Sultani” yaani Rias wa sikuzote kama alivyopendekeza kwenye kauli yake,” amesema.

Aidha amesema, kuwa hatari aliyoiona Mwal. Nyerere bado iko palepale na kuwataka watanzania kupinga utaratibu huo.

error: Content is protected !!