Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa amkabidhi binti mwenye ulemavu nyumba, milioni 18
Habari za Siasa

Majaliwa amkabidhi binti mwenye ulemavu nyumba, milioni 18

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameendesha harambee ya papo kwa papo na kuchangisha Sh.18.9 milioni, kati ya hizo, Sh.10 milioni zimetolewa na Rais John Magufuli ili kumsaidia, Miriam Msagati, binti mwenye ulemavu wa mwili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

“Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli anafuatilia tukio hili na amesema anamchangia Miriam shilingi milioni 10 ili ziweze kumsaidia katika mtaji wa biashara na umaliziaji wa ujenzi wa vyumba vya kupangisha,” amesema Majaliwa

Fedha hiyo ilichangishwa kwa ajili ya Miriam Msagati, binti mwenye ulemavu wa mwili ili ziweze kumsaidia kama mtaji wa biashara na uendelezaji wa ujenzi wa vyumba vya kupangisha katika nyumba ambayo amekabidhiwa leo Ijumaa, tarehe 22 Januari 2021 na Majaliwa.

Gharama ya ujenzi wa nyumba na samani zilizomo ndani ni sh. milioni 47.32.

Majaliwa ameendesha harambee hiyo kwenye kitongoji cha Fune, kata ya Mombo wilayani Korogwe baada ya kumkabidhi binti huyo nyumba aliyojengewa na wadau mbalimbali kutokana na mchango ulioasisiwa na waziri mkuu 5 Machi 2020 alipomtembelea Miriam na kumpatia mchango wa Sh.5 milioni za kuanza ujenzi wa nyumba hiyo.

Waziri Mkuu alimsaidia Miriam baada ya kumsikia binti akimuomba amsaide kupata makazi yeye na bibi yake kupitia kipindi cha Wape Nafasi kinachoongozwa na Tuma Dandi, mtangazaji wa Shirika la Utangazi Tanzania (TBC1).

Baada ya Waziri Mkuu kukabidhi nyumba hiyo, aliwaomba wadau wamchangie Miriam fedha ili apate mtaji pamoja na umaliziaji wa vyumba vya kupangisha ili aweze kujitegemea.

Akiwa bado anaendesha harambee hiyo, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan alizungumza na wananchi hao kupitia simu aliyompigia Waziri Mkuu, ambapo alimpongeza kwa kuhakikisha Miriam anapata makazi bora.

“Nimeona kazi kubwa iliyofanyika hapo, hongereni sana Waziri Mkuu pamoja na uongozi wa mkoa wa Tanga nami namuongezea shilingi milioni tano afanye mtaji.”

Kwa upande wake, Miriam baada ya kukabidhiwa nyumba hiyo alimshukuru Rais Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu kwa uongozi wao wenye kujali wanyonge.

Alisema Tanzania imepata kiongozi mzuri anayewajali wanyonge, hivyo ameahidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awazidishie baraka ili wapate mafanikio mazuri zaidi.

“Siwezi kusahau kitu kama hiki, Mwenyezi Mungu ameniona, Mwenyezi Mungu awabariki watu wote walioshiki katika kufanikisha jambo hili kwani mmeweka hazina yenu kwa Mungu.”

Kwa upande wake, Muandaaji wa Kipindi cah Wape Nafasi, Tuma Dandi alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa namna inavyoshughulikia masuala mbalimbali ya watu wenye mahitaji maalumu.

“Nimeishiwa maneno, leo ni siku nyingine ambayo itaingia katika historia ya maisha yangu. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu na Serikali kwa kufanikisha jambo hili kwani watu wenye ulemavu ni sehemu ya Watanzania ambao wanapaswa kuishi kama wengine.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!