Rais John Magufuli (kushoto) akimkaribisha mgeni wake Dk. Lazarus Chakwera wa Malawi

Magufuli, Dk. Chakwera wazungumzia uchaguzi mkuu

Spread the love

MARAIS John Magufuli wa Tanzania na Dk. Lazarus Chakwera wa Malawi wamezungumzia Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Viongozi hao wamezungumzia uchaguzi leo Jumatano tarehe 7 Oktoba 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam, katika halfa ya kumkaribisha Rais Chakwera, aliyewasili Tanzania kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.

Rais Magufuli amesema, ujio wa marais wa nchi jirani katika kipindi hiki cha kampeni unaashiria baraka za Mungu na ushindi wa uchaguzi huo.

“Nchi yetu imetembelewa na marais watatu wa Burundi, Uganda na sasa Rais wa Malawi, unapoona unatembelewa mara nyingi nyingi ujue hizi ni baraka za Mungu kwamba mambo yanaenda vizuri na hasa unapo ona marais wenzako wanakutembelea unapofanya kampeni, hii inaonesha kwamba wewe ndio utakuwa rais baadae,” amesema Rais Magufuli.

Dk. Lazarus Chakwera wa Malawi

Kwa upande wake, Rais Chakwera amesema, mataifa ya Afrika yanapaswa kutotegemea waangalizi wa kimataifa katika ufuatiliaji wa uchaguzi, kwa kuwa Afrika inaweza kuimarisha demokrasia yake yenyewe.

“Nafikiri ni muhimu kuimarisha demokrasia katika Afrika na lazima tufanye chaguzi zetu bila kuwa na hao waangalizi wa kimataifa sababu wanapokuja waaagalizi hao huwa wanatoa taarifa wanazoamua wenyewe kuzitoa,” amesema Rais Chakwera.

“Kwa hiyo, tuna amini Afrika inaweza kuimarisha demokrasia yake yenyewe na taasisi zake zinafaya kazi vizuri kwa hiyo ni sisi wenyewe kuchukua jukumu letu na si wengine.”

Dk. Chakwera amekuwa wa tatu kuja nchini katika kipindi ambacho kampeni za uchaguzi huo zinaendelea.

Tarehe 13 Septemba 2020 Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliwasili Tanzania na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli wilayani Chato Mkoa wa Geita huku Rais wa Burundi, Evarist Ndayishimiye alitembelea nchini tarehe 19 Septemba 2020 mkoani Kigoma.

Rais John Magufuli

Kuhusu ujio wa Rais Chakwela, Rais Magufuli ameahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi hususan katika sekta ya bandari , kilimo na umeme. Pamoja na kuipa Malawi mbinu za ukusanyaji mapato.

Rais Magufuli amewaahidi wananchi wa Malawi kwamba bandari ya Mtwara na Dar es Salaam itatumika kwa ajili ya kusaidia uchumi wao.

Rais Magufuli amesema ziara hiyo imeleta mapinduzi makubwa na mafanikio na kuwaahidi wananchi wa Malawi wanapokuja Tanzania wajisikie wako nyumba kwa kuwa raia wa mataifa hayo ni wamoja.

MARAIS John Magufuli wa Tanzania na Dk. Lazarus Chakwera wa Malawi wamezungumzia Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea). Viongozi hao wamezungumzia uchaguzi leo Jumatano tarehe 7 Oktoba 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam, katika halfa ya kumkaribisha Rais Chakwera, aliyewasili Tanzania kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu. Rais Magufuli amesema, ujio wa marais wa nchi jirani katika kipindi hiki cha kampeni unaashiria baraka za Mungu na ushindi wa uchaguzi huo. “Nchi yetu imetembelewa na marais watatu wa Burundi, Uganda na sasa Rais wa Malawi, unapoona unatembelewa mara…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!