Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa aipa siku tatu wizara ya kilimo
Habari za Siasa

Majaliwa aipa siku tatu wizara ya kilimo

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa Wizara ya Kilimo kukutana na menejenti ya kampuni ya utengenezaji na usambazaji wa mbolea ya YARA ili kuhakiki na kupata ithibati ya mbolea ya bure itakayogawiwa kwa wakulima wadogo nchini kupitia mpango wa Action Africa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …. (endelea).

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu imesema, majaliwa ametoa wito huo leo Jumatano tarehe 7, Oktoba 7, 2020 alipotembelea kiwanda cha YARA kilichoko jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Majaliwa ameipongeza kampuni ya YARA kwa uwekezaji mkubwa na utekelezaji wa mpango huo wenye thamani ya Sh.16.5 bilioni.

“Serikali inawashukuru sana YARA kwa kutoa mbolea kwa ajili ya wakulima nchini lakini ni muhimu ithibati ifanyike ili iruhusu mbolea iende kwa wakulima.”

“Mpango huu ni mzuri kwa sababu unaendana na malengo ya Serikali katika kukuza sekta ya kilimo hasa uzalishaji wa chakula,” amesema Majaliwa

Majaliwa amesema, Serikali ina nia njema ya kuunga mkono wadau wanaosaidia sekta ya kilimo na amewahakikishia wawekezaji hao usalama na mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini.

Pia, waziri mkuu ametoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kuiga mpango huo wa YARA.

Kadhalika, Majaliwa amemuomba Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elizabeth Jacobsen aanzishe Jukwaa la Biashara kwa Wafanyabiashara wa Tanzania na Norway ili wapata uzoefu wa kibiashara kutoka kila upande.

Kwa upande wake, Mkugenzi Mtendaji wa Kampuni ya YARA, Winston Odhiambo amesema, mpango huo utawanufaisha wakulima wadogo 83,000 nchi nzima ambapo tani 12,500 za mbolea ya zitagawiwa bure kwa wakulima wa mahindi na mpunga.

Odhiambo alisema mpango huo una lengo la kusaidia uzalishaji wa chakula ambapo wanufaika pia watapewa ushauri wa bure kutoka kwa mabwana shamba wa kampuni ya YARA ili kuleta ufanisi katika uzalishaji.

Naye, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Jacobsen amesema mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya dunia kuhusu uhakika wa upatikanqji wa chakula katika bara la Afrika.

Wanufaika wa mpango huu ni wakulima wadogo kwa ajili ya msimu huu wa kilimo ulioanza Septemba hadi Desemba, 2020 ambao tayari wamekwishasajiliwa kupitia mpango huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!