Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli arejesha fomu, milioni 1.02 wamdhamini
Habari za Siasa

Magufuli arejesha fomu, milioni 1.02 wamdhamini

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli amerejesha fomu za kuwania urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rais Magufuli amerejesha fomu hizo leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 makao makuu ya CCM, Dodoma na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Bashiru Ally.

Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, Serikali na wanachama wa chama hicho wakiwemo wenyeviti wa chama hicho nzima waliowasilisha kila mmoja fomu za udhamini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa, Dk. Bashiru amesema, jumla ya wanachama zaidi ya milioni 1 waliojitokeza kumdhamini kutoka mikoa 32 na jumuiya zake tatu za wazazi, vijana na wanawake.

Dk. Bashiru amesema, “fomu nimezipokea na nimedhibitisha kuwa amezijaza vizuri.”

Amesema, leo Jumanne saa 10 jioni ndiyo siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji fomu za urais ndani ya chama hicho. Aliyechukua ni mmoja tu ambaye ni Rais Magufuli.

Rais John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM akizungumza baada ya kurudisha fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya CCM

Mchanganuo wa wadhamini kila mkoa

  1. Arusha – 22,706
  2. Dar es Salaam -71,491
  3. Geita – 89,595
  4. Iringa – 12,542
  5. Kagera – 27,245
  6. Katavi – 5,071
  7. Kaskazini Pemba –2,575
  8. Kaskazini Unguja – 1,141
  9. Kigoma – 30,220
  10. Kilimanjaro – 23,434
  11. Singida – 13,452
  12. Kusini Pemba – 350
  13. Lindi – 9,515
  14. Magharibi Z’bar – 1,005
  15. Manyara –19,972
  16. Mara – 87, 550
  17. Mbeya – 11,600
  18. Mjini Z’bar – 2,394
  19. Morogoro –117,450
  20. Mtwara – 7,566
  21. Njombe – 17,810
  22. Pwani – 20,603
  23. Rukwa – 5,600
  24. Ruvuma – 56, 350
  25. Shinyanga – 12,000
  26. Simiyu – 3,693
  27. Songwe – 11,744
  28. Tabora – 29,489
  29. Tanga – 62,839
  30. Mwanza –
  31. Kusini Unguja –

 32.Dodoma – 44, 415

Jumuiya za chama

  1. UWT – 66,633
  2. Wazazi – 48,329
  3. UVCCM – 100,360

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!