Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Madereva 3 wafungiwa milele kuendesha magari nchini
Habari Mchanganyiko

Madereva 3 wafungiwa milele kuendesha magari nchini

Spread the love

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limewafutia leseni za udereva wadereva watatu na kuwafungia milele kuendesha magari aina ya mabasi pamoja na yale ya mizigo kwa kosa la kusababisha ajali na vifo, anaandika Faki Sosi.

Kadhalika, madereva saba wamefutiwa leseni zao za daraja ‘C’ na ‘E’ kwa makosa ya kuendesha kwa kasi zaidi ya kilometa 90 kwa saa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamanda wa Kikosi hicho Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Fortunatus Musilimu amesema madereva hao hawaturuhusiwa kuendesha gari za abiria au mizigo kwa muda wa miezi sita.

Musilimu amesema madereva hao wanatakiwa kurudi darasani, kusoma upya na kupewa mitihani na kama watafaulu watapewa leseni upya.

Amewataja madereva hao kuwa Hamadi Salumu mwenye Leseni namba 4001852854, Kija Mayenga (4001518000), Issack Mbijina (4000220395), Hassan Semazua (4001522366), Stanley Mosha (4000369436).

Wengine Abdallah Husseni (4000482412) ambaye hadi sasa yupo mahabusu kwa kushindwa kulipa fainin na Sempunda Yusufu (1-1980,80006518226).

Madereva waliofungiwa kuendesha magari milele ni pamoja na Ismail Nyami, mwenye leseni 4000676285 ambaye alisababisha ajali Septemba 23, mwaka huu iliyoua watu wawili, na kujerehi 42 wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, na Mseka Salumu, (4000118648) aliyesababisha ajali Septemba 25 mwaka huu iliyoua mtu mmoja na kujeruhi 25 eneo la Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga

Mwengine ni Malik Hassani (4000450337) aliyesababisha ajali Septemba 21 mwaka huu na kuua mtu mmoja na kujeruhi sita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!