Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mashishanga atoa neno migogoro wakulima, wafugaji
Habari Mchanganyiko

Mashishanga atoa neno migogoro wakulima, wafugaji

Stephen Mashishanga
Spread the love

WAKAZI wa kata mbalimbali wilayani Mvomero mkoani Morogoro wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Chama cha Waandishi wa Habari (MOROPC), ili kuboresha shughuli za kupambana na kutokomeza migogoro ya ardhi inayowahusu wakulima na wafugaji wa wilayani humo, anaandika Christina Haule.

Akizungumza kwenye warsha ya siku tatu iliyohusisha watendaji wa vijiji, mitaa na vitongoji katika kata tatu za Hembeti, Dakawa na Mvomero aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Stephen Mashishanga amesema migogoro inaweza kutatuliwa ikiwa wakazi wa eneo husika wataonesha ushirikiano.

Aidha, aliwataka wakazi hao kutambua kwamba kuna watu wanatumia migogoro kujinufaisha na kuwaacha wengine wakitaabika kutokana na vifo, majeruhi na majanga ya njaa.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imelenga kumaliza migogoro ya ardhi ambayo imeisumbua nchi kwa miaka 50 sambamba na kuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo.

“MOROPC imeona umuhimu wa suala la utatuzi wa migogoro ya ardhi na kufadhiliwa na The Foundation For Civil Society (FCS), ili kuunga mkono serikali na kuleta amani ambayo ndio njia ya maendeleo” amesema Mashishanga ambaye pia ni Mlezi wa MOROPC.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Morogoro, Omary Mbega amesema sheria namba ya ardhi ya mwaka 2002 inazungumza nama chombo hicho kinavyoweza kupata ufumbuzi.

Mbega amesema kuwa migogoro mingi inayotokea ndani ya vijiji inatokana na baadhi ya viongozi wake kushindwa kufuata sheria na kuamua kuuza ardhi ya wananchi mara mbili.

“Naombeni viongozi wenye tabia kama hii kuacha mara moja na badala yake wafuate sheria ya ardhi inasemaje” amesema Mbega.

Mmoja wa wananchi walioshiriki mafunzo hayo, Anna John kutoka kata ya Hembeti amesema kuwa uelewa mdogo wa wananchi juu ya umilikaji ardhi kisheria umesababisha waporwe ardhi yao.

Mafunzo hayo yanayotekelezwa na Klabu ya waandishi wa habari mkoani Morogoro yamefadhiliwa na Shirika la The foundation for Civil Society.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!