Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa kuanika kilichomkimbiza Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Lowassa kuanika kilichomkimbiza Chadema

Spread the love

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa, yuko mbioni kueleza ulimwengu, kilichomsukuma kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Nitaeleza, tena silo muda mrefu, kilichonitoa Chadema na kunijeresha CCM. Nitazungumza. Nitafanya hivyo muda si mrefu,” ameeleza Lowassa ambaye IJumaa iliyopita, aliondoka ghafla katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kurejea CCM.

Lowassa alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho; katika  uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015, Chadema kikiungwa mkono na jumuiko la vyama vilivyoko katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vilimfanya mwanasiasa huyo kuwa mgombea wake wa urais.

Alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais John Pombe Magufuli. Hata hivyo, Lowassa mwenyewe amekuwa akidai mara kadhaa kuwa kura zake ziliibwa.

Mbali na Chadema, vyama vingine vilivyomuunga mkono Lowassa, pamoja na Chama cha Wananchi (CUF), NCCR- Mageuzi na National League Democrat (NLD).

Akizungumza na gazeti moja la kila siku, Lowassa amesema, “Watanzania watulie. Wasiwe na shaka kutokana na uamuzi wangu wa kuondoka Chadema. Nitaweka wazi kila kitu kilichosababisha kuachana na chama hicho.”

Alisema, “maswali yote uliyonayo, nitayajibu kupitia mkutano wa waandishi wa habari nitakaouitisha muda wowote kuanzia sasa. Usiwe  na wasiwasi. Utajulishwa na nitazungumza yote unayoyahitaji kuhusu mimi.”

Akiongea katika ofisi za ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuingia mkataba mpya na CCM, Lowassa alisema, ameamua kurejea nyumbani ambako sehemu kubwa ya maisha yake yamekuwa huko.

Lowassa alikihama CCM na kujiunga na Chadema, kupitia mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika tarehe 28 Julai 2015, katika Hoteli ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam.

Alichukua hatua hiyo, wiki moja baada ya jina lake kuenguliwa katika orodha ya wagombea urais wa CCM.

Katika mkutano huo, Lowassa aliwaeleza waandishi wa habari kuwa CCM haikumtendea haki katika kupitisha majina ya wagombea urais, hivyo hawezi kuendelea kubaki kwenye chama kisichokuwa na kuheshimu demokrasia.

Alisema, “niliwekewa mizengwe, kuhakikisha jina langu halifiki Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC). Nia yangu ni kuleta mabadiliko na kuondoka kwangu na kujiunga na Chadema, ni kuendeleza dhamira hiyo,” alieleza kwenye mkutano huo.

Alisema, “CCM siyo Baba yangu, wala siyo Mama yangu. Kama Watanzania wameyakosa mabadiliko CCM, basi watayatafuta kwingine. Ninaondoka. Sijakurupuka.”

Tofauti na utamaduni wa Lowassa wa kusindikizwa na familia yake na watu wake wa karibu katika kufanya maamuzi mengi ya kisiasa, safari hii, alisindikizwa na aliyekuwa “swahiba wake mkubwa,” Rostam Aziz.

Rostam ni mmoja wa waliopata kuwa viongozi wajuu wa chama hicho na mbunge katika jimbo la Igunga, mkoani Tabora.

Aliwahi kujiuzulu uongozi, ikiwamo ujumbe wa NEC na ubunge na baadaye kujiweka mbali kwenye siasa za nchini, kufuatia kuandamwa na shutuma kadhaa za ufisadi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!