December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Radi zatawala maziko ya Ruge

Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba ukiwa nyumbani kwao Bukoba

Spread the love

TARATIBU za kukamilisha shughuli ya mazishi ya Ruge Mutahaba, mwanahabari aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya Clouds Media Group (CMG) yametawaliwa na mvua pia radi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Bukoba … (endelea).

Mwili wa Ruge utazikwa leo Jumatatu mchana tarehe 4 Machi 2019 kijijini kwao Kizuri, Bukoba mkoani Kagera baada ya shughuli zote kukamilika.

Wakati shughuli hizo zikiendela, mvua imeendelea kunyesha sambamba na radi tofauti na siku zilizopita. Shughuli za mwisho za kuuaga mwili wa Ruge zitafanyika katika viwanja vya Gymkhana, Bukoba.

Mwili wa Ruge ulitangulia kuagwa juzi tarehe 2 Machi 2019 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karimjee ambapo viongozi wa taasisi, mashirika, wanasiasa na viongozi mbalimbali wa kitaifa waliongozwa na Rais John Magufuli.

Ruge alifariki dunia tarehe 26 Februari 2019 nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu ya figo lililomsumbua kwa zaidi ya miezi mine. Alianza kutibiwa katika Hospitali ya Kairuki iliyoko jijini Dar es Salaam na baadaye alipelekwa India kishakupelekwa Afrika Kusini ambako umauti ulimfika.

error: Content is protected !!