Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Mvua yaleta kizazaa Dar
Habari MchanganyikoTangulizi

Mvua yaleta kizazaa Dar

Spread the love

MVUA kubwa imenyesha jiji Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumapili na bado inaendelea “kupiga” katika maeneo kadhaa jijini hapa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa kutoka maeneo mbalimbali za jiji hili zinasema, mvua nyingi imenyesha katika maeneo ya Kariakoo, Jangwani, Ilala, Kinondoni Bunju hadi Bagamoyo.

“Ukanda wote huu wa Pwani, mvua kubwa imenyesha na kwa mujibu wa taarifa ya hali hewa, mvua hizo zitaendelea kunyesha hadi Mei mwaka huu,” ameeleza mtaalam mmoja kutoka Idara ya hali hewa.

Mtaalam huyo ambaye hakupenda kutajwa jina kwa kuwa siyo msemaji wa Idara hiyo anasema, “utabiri unaonyesha kuna mvua kubwa zinazoweza kunyesha na huenda zikaleta maafa.”

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia magari kadha yakiwa yamekwama kwenye maji maeneo ya Kariakoo na Jangwani.

“Hapa Jangwani, kote kumejaa maji. Katika eneo la magari ya Mwendokasi, maji yamejaa na kuathiri kwa kiwango kikubwa usafiri,” ameeleza mmoja wa mashuhuda.

Katika eneo la Kariakoo, hasa barabara ya Nyerere aneo la Gerezani, magari kadhaa yalikwama na mengine kuzimika.

Kufuatia hali hiyo, baadhi ya vijana wanaofanya biashara ndogo ndogo katika maeneo hayo, walitumia fursa ya mkwamo; na au kuzimika wa magari hayo, kujipatia ajira.

Wengi wao walijitosa barabarani na kuanza kusaidia kukwamua baadhi ya magari yaliyokwama.

Kioja kikubwa kilikuwa pale gari la wagonjwa – Ambulance – lilizimika.

Baadhi ya vijana waliombwa kusaidia kulikwamua gari hilo, walilikwepa kwa hoja kuwa “mgonjwa hana hela.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!