Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu atinga Kariakoo kwa mwendokasi
Habari za SiasaTangulizi

Lissu atinga Kariakoo kwa mwendokasi

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema alipotembelea sokoni Kariakoo
Spread the love

TUNDU Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameahidi kuliboresha Jiji la Dar es Salaam, endapo atashinda Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ametoa ahadi hiyo leo tarehe 7 Oktoba 2020 alipotembelea maeneo ya Kariakoo jijini humo huku akilakiwa na mamia ya wananchi waliokuwepo kwenye maeneo hayo.

Mwanasiasa huyo amewaomba wakazi wa Dar es Salaam kumchagua ili aliboreshe jiji hilo liwe la kisasa.

“Wakazi wa Dar es Salaam wana kila sababu ya kuniunga mkono sababu tunataka jiji la kisasa, jiji letu linahitaji mabadiliko makubwa, kuna tatizo kidogo kwa mtu asiyetembea, ukiuliza jiji hili lenye watu zaidi ya milioni tano  wapi mahali watu wanapumzikia hakuna, nashangaa,” amesema Lissu.

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema alipotembelea sokoni Kariakoo

Aidha, Lissu ameahidi kuboresha mfumo wa usafirishaji abiria na bidhaa, kwa kutanua mtandao wa barabara, kujenga njia za reli za juu na chini na usafiri wa majini.

“Nataka tuwe na maeneo maalum kwa ajili ya mwendokasi na iende kila mahali, hauwezi tatua  tatizo la usafiri kwa kufanya vitu kidogo kidogo.”

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema alipotembelea sokoni Kariakoo

“Unawaonjesha hapa, unawaonjesha pale haiwezekani, lazima tuwe na mfumo wa usafiri  kuangalia usafiri wa majini, reli za juu na chini, usafiri wa mabasi, ndiko tunakoelekea,” amesema Lissu.

Lissu anayetumikia adhabu ya kutofanya mikutano ya kampeni kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 3 hadi 9 Oktoba 2020 kw a kosa la kukiuka kanuni za maadili ya uchaguzi, ametembelea Kariakoo majira ya mchana, ambapo amezungumza na wananchi mbalimbali.

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema akiwa ndani ya basi la Mwendokasi akielekea Kariakoo

Mwanasiasa huyo ametumia usafiri wa Mwendokasi kufika Kariakoo ambapo kila alipopita aliibua shangwe ambapo amefanya manunuzi ya bidhaa kadhaa ikiwemo mchele.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!