Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aachiwa huru, simu zake zashikiliwa
Habari za SiasaTangulizi

Lissu aachiwa huru, simu zake zashikiliwa

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema (katikati) akizungumza na vyombo vya habari muda mchache baada ya kutoka kuhojiwa na polisi
Spread the love

HATIMAYE Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kufutiwa mshitaka na kukamatwa tena leo asubuhi kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kidini, anaandika Charles William.

Lissu alikamatwa akiwa ndani ya Mahakama ya Kisutu baada ya serikali kuwasilisha taarifa kuwa haina nia ya kuendelea na kesi iliyofungua hapo awali na kisha polisi kumpeleka kituo ch kati kwa mahojiano.

Taarifa zilizopatikana leo jioni zinaeleza kuwa Lissu amehojiwa juu ya kauli yake aliyoitoa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar miezi miwili iliyopita pale alipotamka kuwa “Uchaguzi w Zanzibar ulikuwa haramu kama muislam kula nyama ya nguruwe.”

Hata hivyo inadaiwa kuwa Lissu ameachiwa lakini simu zake za mkononi zimeendelea kushikiliw na polisi na kwamba atatakiwa kuripoti tena manmo tarehe 13 Machi mwaka huu katika kituo cha polisi cha kati.

Mapema leo asubuhi baada ya kukamatwa Lissu alindika ujumbe ukisema, anaamini kukamatwa kwake kuna uhusiano wa moja kwa moja uchaguzi ujao wa Chama cha Mawakili hapa nchini (TLS), unaotarajia kufanyika wiki mbili zijazo.

“Serikali hii, kwa kutumia mawakili wao vibaraka, imekuwa na mkakati mkubwa wa kunizuia kugombea urais wa TLS. Walipanga kwenda kupinga kugombea kwangu mahakamani. Tumewasema hadharani na kuzianika njama zao. Sasa wameamua kutumia rungu lao la siku zote,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!