Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ataka wananchi wadhibiti ufisadi
Habari za Siasa

Mbunge ataka wananchi wadhibiti ufisadi

Kunti Yusuph Majala, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema)
Spread the love

KUNTI Yusuph Majala, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) mkoa wa Dodoma, amewataka wananchi kujenga tabia ya kuhoji ubora na uendeshwaji wa miradi ya kata na vijiji ambayo hutengewa fedha na halmashauri, anaandika Dany Tibason.

Kunti ametoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Berega, kitongoji cha Nghambi wilayani  Mpwapwa, Dodoma.

Pia alijibu maswali ya wananchi juu ya matumizi na utolewaji wa fedha ambazo zinatakiwa kutolewa na halmashauri ikiwemo asilimia tano kwa ajili ya vijana na asilimia tano ya wanawake.

“Zipo fedha ambazo hutengwa na halmashauri kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini fedha hizo haziwezi kupatikana bila kuwepo kwa vikundi ambavyo vimesajiliwa pamoja na wananchi kutimiza wajibu wa kuhoji utolewaji wa fedha hizo.

“Wananchi ndiyo mnaishi kwenye kata na vijiji ambavyo miradi ya maendeleo inatekelezwa, ni lazima mpewe taarifa kwa viongozi wenu juu ya miradi hiyo na muangalie kama inaendana na thamani ya fedha pia lazima asilimia tano ya wanawake na vijana iwafikie kupitia vikundi vyenu,” amesema.

Katika hatua nyingine wananchi wamelalamikia huduma mbovu ambazo hutolewa katika zahanati ya Nghambi, licha ya wananchi hao kuwa wamejiunga na mfuko wa afya ya jamii (HCF).

Ibrahim Maswaswa, miongoni mwa wananchi waliohudhuria mkutano wa Mbunge huyo alisema wananchi wanachangia fedha nyingi katika mfuko wa bima ya afya lakini hakuna huduma yoyote ambayo inapatikana katika zahanati hiyo jambo ambalo linawafanya wananchi kukosa huduma ya uhakika.

“Zahanati yetu haina madaktari na badala yake kuna manesi wawili tu ambao utendaji wao hauwezi kukidhi kiwango cha utoaji wa huduma kwa wananchi wa kitongoji kizima,” amesema Ibrahim.

Kutokana na hali hiyo wananchi walimuomba mbunge kupeleka kilio hicho bungeni ili katika Bajeti ijayo ya serikali zahanati hiyo iweze kuongezewa watumishi pamoja na kuwepo kwa dawa za kutosha tofauti na ilivyo sasa. Mbunge alikubaliana na ombi hilo la wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!