Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kisa bando la intaneti, TCRA yapewa siku 90
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kisa bando la intaneti, TCRA yapewa siku 90

James Kilaba, Mkurugenzi wa TCRA
Spread the love

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (Tehama) nchini Tanzania, Dk. Faustine Ndugulile, ameipa miezi mitatu (siku 90), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kumaliza changamoto za bando (vifurushi), zinazotolewa na kampuni za simu za mkononi kwa wananchi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Ndugulile ameyasema hayo hivi karibuni alipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam ambapo  amezungumza na Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Amesema, TCRA ishughulikie malalamiko ya wananchi kwa kuwa wananchi hawana imani na vifurushi na kuwe na mfumo wa kuhakiki gharama halisi za mawasiliano kuendana na fedha aliyotoa mwananchi.

Dk. Faustine Ndugulile, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (Tehama) nchini Tanzania,

Waziri huyo amesema, kuwe na namba ya bure ambayo wananchi watapiga ili kuwasilisha malalamiko yao ili kuwawezesha wananchi kuongeza imani yao kwa Serikali.

Amesisitiza ni heri tufanye maamuzi mabaya kuliko kutokufanya maamuzi na amewataka washirikiane na Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA – CCC), kumaliza changamoto hiyo kwa kuwa, Watanzania sio wajinga, anataka aone kapata shilingi moja anaitumia shilingi moja yake kupiga simu.

Pia, amehimiza wahakikishe chaneli tano za bure za runinga zinaonekana hata baada ya muda wa kulipia kumalizika kwa kuwa chaneli hizo hazionekani kwenye baadhi ya ving’amuzi.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew ameipongeza TCRA kwa kutengeneza mifumo ya TEHAMA, kutambua changamoto zilizopo na imejipanga kuzifanyia kazi kwa kuwa lazima TEHAMA ichukue nafasi yake na itufikishe Watanzania tunakotaka kwenda.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Zainab Chaula amewataka wafanyakazi wa TCRA kujiongeza na kujituma zaidi badala ya kusubiri maagizo na maelekezo kwa kuwa wao ni wataalamu, hivyo washirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwahudumia watoa huduma na watumiaji wa huduma za mawasiliano.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amekiri uwepo wa changamoto za vifurushi na ameahidi kuzifanyia kazi kwa kuwa TEHAMA imeongeza mnyororo wa thamani kwenye sekta zote na imesogeza huduma mbali mbali viganjani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!