Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kikwete: JPM amewazima midomo wapinzani ajenda ya rushwa
Habari za Siasa

Kikwete: JPM amewazima midomo wapinzani ajenda ya rushwa

Spread the love

MWENYEKITI mstaafu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Mrisho Kikwete amesema, Rais wa Tanzania anayemaliza muda wake, John Magufuli amewazima midomo wapinzani juu ya ajenda ya rushwa na ufisadi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kikwete ameyasema hayo leo Jumamosi tarehe 17 Oktoba 2020 wakati anamuombea kura Rais Magufuli ambaye ni Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Zakhiem-Mbagala Dar es Salaam.

Rais huyo mstaafu wa Tanzania wa Serikali ya awamu ya nne, amesema katika uongozi wa Rais Magufuli amefanikiwa kupambana na rushwa pamoja na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi, kiasi kwamba wagombea wa upinzani wameshindwa kuitumia ajenda hiyo katika mikutano ya kampeni.

“Rais Magufuli kapambana na rushwa, mahakama ya mafisadi imeanzishwa ndio manaa uchaguzi huu sijasikia mgombea yeyote aliyezungumza rushwa na atakeyechukua kama ajenda atakua ameishiwa,” amesema Kikwete.

Kikwete amewaomba wananachi wa Temeke na Mbagala wamchague tena Rais Magufuli ili amalize kazi aliyoianza katika awamu yake ya kwanza ya uongozi, ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya na hospitali, barabara, usambazaji maji na umeme na huduma nyingine za kijamii.

“Tumchague Magufuli aendelee kuongoza nchi yetu, tumpe miaka mitano mingine amalize ngwe yake. CCM ina sera nzuri za kudumisha masilahi ya kisiasa, kijamii, kitamaduni, kiusalama na watu wake. Hakuna chama kingine kinachofanana na CCM mimi sikijui,” amesema Kikwete.

Wakati huo huo, Kikwete amewaomba Watanzania kuchagua wagombea wa CCM akisema kwamba chama hicho kina sera nzuri zinazodumisha amani, umoja na muungano wa Taifa.

Pamoja na kuwa na Ilani zenye kutatua changamoto za Watanzania.

“Sera nzuri za CCM zimeliunganisha taifa la Tanzania, zimejenga umoja, udugu, upendo miongoni mwa watu na wananchi wa Tanzania. Sababu ya pili ya kutaka CCM ichaguliwe tena kuongoza nchi yetu, imekuwa inatengeneza ilani za uchaguzi zinazotambua changamoto zinazokabili wananchi wa Tanzania,” amesema Kikwete.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!