May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Liverpool yabanwa mbavu

Spread the love

BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu nchini England klabu ya Liverpool imelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton kwenye mchezo wa Ligi nchini humo uliochezwa majira ya saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Goodson Park. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Liverpool imeambulia pointi moja katika michezo miwili ya Ligi kuu nchini humo mara baada ya kupoteza katika mchezo uliopita dhidi ya Astorn Villa.

Mabao ya Liverpool kwenye mchezo huo yalifungwa na Sadio Mane dakika ya 3 na Mohammed Salah 71’ ambaye amefikisha mabao 100 toka alipojiunga na Liverpool.

Kwa upande wa Everton mabao yao yalipatikana dakika ya 19 na Kean, na baadae dakika ya 81’ Calvert Lewin akaisawazishia timu yake na mchezo kumalizika sare.

Kwa matokeo hayo Liverpool itakuwa na alama 10 na kusogea nafasi ya pili huku Everton ikiendelea kusalia kileleni kwenye msimamo huo kwa kuwa na pointi 13 baada ya kucheza michezo mitano.

error: Content is protected !!